SIMBU APANDISHWA CHEO BAADA YA KUNG’ARA TOKYO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 25, 2025

SIMBU APANDISHWA CHEO BAADA YA KUNG’ARA TOKYO


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda amempongeza Sajini Alphonce Simbu kwa ushindi wa medali ya dhahabu katika Mashindano ya Mbio za Marathon ya Dunia Kilomita 42, zilizofanyika Tokyo Japan.

Pamoja na pongezi hizo, Jenerali Mkunda amempandisha cheo kutoka Sajini kuwa Sajinitaji tukio lililofanyika ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi Upanga Jijini Dar es Salaam leo Septemba 25, 2025.

Jenerali Mkunda amesema ushindi huu ni kwa Watanzania wote na Afrika kwa ujumla na kwamba michezo ni sehemu ya kazi jeshini, hivyo Sajinitaji Alphonce Simbu amefanya kazi nzuri.

Jenerali Mkunda ametoa rai kwa maafisa na askari wote jeshini kuiga mfano wa Sajinitaji Simbu kwa kufanya kazi kwa bidii na kuleta mafanikio katika kila idara jeshini.

No comments:

Post a Comment