Mgombea Ubunge wa Jimbo la Pangani Mkoani Tanga ambaye pia ni Waziri wa Maji kwenye serikali ya awamu ya sita Mhe. Jumaa Aweso amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi na uthubutu wake wa kujenga tenki kubwa la maji la Bangulo linalohudumia wananchi wa Halmashauri za Ubungo, Kisarawe, Temeke na Jiji la Ilala Mkoani Dar Es Salaam.
Aweso ametoa shukrani hizo leo Jumatano Oktoba 22, 2025 kwenye Viwanja vya Kecha, Kinyerezi Wilayani Ilala wakati wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema kabla yake maeneo ya Segerea, Kivule, Ukonga na Ubungo yalikuwa na changamoto kubwa ya maji, suala ambalo lilimfanya kufanya ziara katika eneo hilo mara kwa mara.
"Huwa najiuliza sana hali ingekuwaje leo kama Dkt. Samia asingefanya maamuzi ya ujenzi wa Tenki hili la Bangulo. Kazi ya sasa iliyopo ni kuwaunganishia wananchi maji wa Segerea, Ukonga na Kivule.
"Na nisema kuwa hapa nina salamu zenu wananchi wa eneo hili kutoka kwa Dkt. Samia. Anatambua kuwa tenki hili limekamilika, wananchi wameteseka kwa muda mrefu, maelekezo aliyoyatoa ni wananchi wa eneo hili kwamba nenda kwa Meneja wa Dawasa kama huna hela ya kuunganishiwa maji, utaunganishiwa na utalipa kidogo kidogo kwenye bili yako. Huyo ndiyo Dkt. Samia na meneja yeyote akikuzingua, piga simu nizinguane naye." Amesisitiza Mhe. Aweso.
Mradi wa Bangulo unahusisha Halamshauri za Ubungo, Kisarawe, Temeke na Jiji la Ilala ikiwa ni juhudi za Serikali katika kuboresha huduma ya upatikanaji wa majisafi kwa wakazi 450,000 wa Dar es Salaam ya Kusini na kugharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 36,967,122,894.44, ukisafirisha na kusambaza maji kwa wananchi wa Ukanda huo kwa kiasi cha lita Milioni 23.3 kwa siku.qa
No comments:
Post a Comment