
Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Temeke Mkoani Dar Es Salaam kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mariam kisangi amemshukuru Mgombea wa nafasi ya Urais wa Tanzania na Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya Bilioni 18 kwaajili ya miradi ya maendeleo Temeke pamoja na shilingi Bilioni 43.6 zilizotolewa kwenye ujenzi wa miundombinu ya usafiri na usafirishaji katika Jimbo hilo.
Kisangi amebainisha hayo leo Alhamisi Oktoba 23, 2025 kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais Dkt. Samia katika Wilaya hiyo kwenye Viwanja vya Tanesco Buza akisema Bilioni 43.6 za ujenzi wa miundombinu zimetolewa kupitia Mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam (Dar es Salaam Metropolitan Development Project – DMDP).
Kupitia Mradi huo Kisangi amesema utaongeza mtandao wa barabara za lami kwa Kilomita 16.38 pamoja na vivuko sita, mradi ukitarajiwa kugusa Kata kumi za Jimbo la Temeke ikiwemo ujenzi wa barabara ya Voda- Kipera pamoja na barabara nyingine zitakazojengwa kwa fedha za ndani kupitia TARURA ikiwemo barabara ya Mashine ya maji- Azimio, barabara ambayo imekuwa kero kubwa kwa muda mrefu kwa wananchi wa eneo hilo.
No comments:
Post a Comment