
"Twendeni tukachague Chama cha Mapinduzi ili tujenge nchi yetu, msidanganywe na watu wengine na niwaambie kuwa kwa sasa hakuna chama kingine kitakachoweza kuendesha nchi hii kisha yakapatikana maendeleo yaliyopatikana sasa. Ni Chama Cha Mapinduzi pekee ndicho kilichoijenga nchi hii na ndicho kinachoweza kuijenga nchi na kikawaletea maendeleo na ndicho Chama kilichoachiwa misingi na falsafa za kisiasa na kisera na waasisi wa Taifa hili akiwemo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage" - Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea wa nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara leo Ijumaa Oktoba 10, 2025.



No comments:
Post a Comment