
Oktoba,10 , 2025 Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mh.Janeth Massesa - PRM katika shauri la Rushwa namba 24775/2025 imemtia hatiani Mkulima Bw. Anthony Mutagwaba Kagombora, kwa tuhuma za Rushwa.
Chini ya kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya 2023, Mkulima huyo kwa njia ya rushwa alijipatia kiasi cha Tshs. 1,626,570 kutoka Chama cha Ushirika KIHUMULO AMCOS ikiwa ni malipo ya kahawa aina ya Robusta msimu wa mwaka 2024/2025, huku akijua yeye sio mwanachama na hakuuza kahawa katika chama hicho kwa kipindi cha mwaka 2024/2025 .
Baada ya Mshtakiwa kutiwa hatiani ametakiwa kulipa fine ya Tsh. 500,000 au kwenda Jela mwaka Mmoja, na kutakiwa kurejesha kiasi cha Tsh. 1,626,570/- kwenye Chama cha Ushirika KIHUMULO AMCOS ndani ya miezi mitatu.
Mshtakiwa amelipa faini.
Shauri hili liliendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Daudi Jacob Oringa.
TAKUKURU (M) Kagera Oktoba 10, 2025
No comments:
Post a Comment