SAMIA SIO FISADI, TUMETHIBITISHA HILO WANAWAKE WA MARA- AGNES MARWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 9, 2025

SAMIA SIO FISADI, TUMETHIBITISHA HILO WANAWAKE WA MARA- AGNES MARWA



"Nasimama mbele yenu ndugu zangu kwa heshima na taadhima naombeni kura zenu zote kwa Mama yetu Samia Suluhu Hassan, ni mwanamke aliyetuheshimisha wanawake. Mama Samia sio fisadi, Mama Samia sio mwizi na ndio maana wanawake wa Mkoa wa Mara tunathubutu kusema mitano tena inakustahili Mama.

Tulikwenda wanawake kutoka kila Kata za Mkoa wa Mara nyumbani kwa Mama Samia anapoishi yeye na Mama yake mzazi. Tulikwenda kuangalia, na wanawake wa kila Kata za Mkoa wa Mara ni mashuhuda Mama, walidhani watakutana na maghorofa, wanawake wakakuta nyumba anayoishi Mama yako mzazi, Mhe. Mwenyekiti wetu ni kama nyumba anayoishi Mama yangu mimi, Muuza dagaa."- Agnes Marwa, Mbunge mteule wa viti Maalum Mkoa wa Mara, akizungumza kwenye Kampeni za Dkt. Samia Suluhu Hassan Musoma Mjini leo Oktoba 09, 2025.


No comments:

Post a Comment