
"Niwahakikishie tarehe 29 keshokutwa mwezi huu wa kumi, niwaombe tokeni nendeni mkapige kura. Ninayeongea hapa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi hii, nataka niwaambie maandamnao yatakayokuwepo ni ya watu kwenda vituoni kupiga kura. Hakuna maandamano mengine yatakayokuwepo, hakuna tishio la kiusalama litakalokuwepo. Anayesema ni Amiri Jeshi Mkuu wa nchi hii, niwaombe ndugu zangu twendeni tukapige kura.
"Ndugu zangu mengine niachieni mimi, matusi niachieni mimi, nayabeba kwaajili yenu. Manabii wetu akiwemo Bwana Yesu alisulubiwa kwa kukomboa watu kwa amri ya Mungu lakini alikuwa anafanya kazi ya watu, Nabii Muhammad alipigwa mpaka akatolewa meno kwa kufanya kazi ya kukomboa watu kwa amri ya Mungu.
..Samia Suluhu aliapa kuitumikia Tanzania na ndicho ninachokifanya. Niliapa kuilinda nchi, Niliapa kujenga na kuheshimisha utu wa Mtanzania na ndicho ninachokifanya. Kwahiyo sina uchungu ndugu zangu wa kubeba matusi yote yanayotolewa kwasababu nafanya kazi hii, sina uchungu, sijutii kwahiyo niwaombe sana ndugu zangu wa Wilaya hizi mbili za Ubungo na Kinondoni mtupe kura."- Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea wa nafasi ya Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi akiomba kura kwa wananchi wa Kinondoni kwenye Viwanja vya Leaders Club leo Jumanne Oktoba 21, 2025.
No comments:
Post a Comment