"Mkoa wetu huu wa Rukwa una utajiri mkubwa sana wa madini ikiwemo makaa ya mawe, Vito, dhahabu na shaba ipo hapa ndani ya Rukwa na tunaendelea kufanya utafiti kuhusu madini hayo. Kwasasa niseme tu kwamba Mkoa wa Rukwa ina soko la madini pamoja na vituo sita vya ununuzi wa madini na tunapozungumza leo Mkoa wetu umepata wawekezaji takribani kumi, wameonesha ishara ya kuja kuwekeza kwenye madini hapa Mkoani Rukwa na majadiliano bado yanaendelea.
Sambamba na kujitokeza kwa wawekezaji hao kipaumbele chetu cha kwanza ni wachimbaji wadogo, Vijana wa Rukwa ambao tutawatengenezea mpango wafanye kazi kwa pamoja na hawa wachimbaji wakubwa wanaokuja.
"Lakini vilevile tunaangalia uwezekano wa kuanzisha Kiwanda kikubwa cha kuchakata shaba hapa Rukwa, bado tupo kwenye mazungumzo, wanaoitaka shaba yetu ya Rukwa wamekuja kuangalia, wameona, tupo kwenye mazungumzo waweke kiwanda hapa hapa, ichakatwe hapa, Vijana wetu wapate ajira na ndiyo maana tunajenga Vyuo vya VETA vijana wafundishwe wakafanye kazi kwenye Viwanda vya aina hii ili badala ya wao kubeba udongo wetu wa shaba wafakanye kwao, wafanye hapa ili Vijana wetu wapate ajira."- Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi akizungumza na wananchi wa Sumbawanga Mjini Mkoani Rukwa kwenye Viwanja vya Kizitwe leo Oktoba 19, 2025.


No comments:
Post a Comment