MWANDISHI WA UHURU, MZALENDO AJITOSA UNAIBU MEYA MOROGORO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, November 20, 2025

MWANDISHI WA UHURU, MZALENDO AJITOSA UNAIBU MEYA MOROGORO



Na Shua Ndereka, Morogoro


Zoezi la uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi ya Umeya na Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) limefunguliwa rasmi huku mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru na Mzalendo, ambaye ni Diwani wa viti maalum kupitia UWT mkoani Morogoro Mhe. Latifa Ganzel, akiwania nafasi ya Naibu Meya.

Akizungumzia zoezi hilo, Katibu wa Umoja wa Vijana(UVCCM) Wilaya ya Morogoro mjini Khalid Hossein King amesema kuwa, zoezi hilo linatarajiwa kukamilika Novemba 21 majira ya saa kumi jioni huku muitikio ukiwa mkubwa kwa wanachama waliojitokeza kuchukua fomu hizo.

Mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Unaibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Diwani wa Viti Maalum Mhe. Latifa Ganzel, amesema baada ya kulitumikia Baraza la Madiwani kwa muda wa miaka 10 ameona ni wakati muafaka wa kugombea nafasi hiyo ili kuongeza vyanzo vipya vya mapato ikiwa ndicho kipaumbele chake kikubwa.

No comments:

Post a Comment