PSSSF yakutana na vyombo vya habari Tabora, yawajengea uelewa juu ya Mafao na huduma zake - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 25, 2025

PSSSF yakutana na vyombo vya habari Tabora, yawajengea uelewa juu ya Mafao na huduma zake


Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umezidi kuendeleza uhusiano mazuri na vyombo vya habari kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi ili waweze kuripoti vyema masuala mbalimbali ya Hifadhi ya Jamii ambapo Novemba ilikutana na waandishi mkoani Tabora.

Kikao hicho na Waandishi wa habari wa mkoani Tabora kilifanyika chini ya uratibu wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoani Tabora (TPC) ambapo Mwenyekiti wa klabu hiyo Bw. Juma Kapipi aliishukuru PSSSF kwa kuandaa kikao hicho muhimu kwa waandishi wa habari mkoani Tabora.

Viongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tabora (TPC) wakiwa katika picha ya pamoja wa watendaji wa PSSSF, baada ya mafunzo yaliyoandaliwa na Mfuko kwa ajili ya wanachama wa TPC

“Kwa kweli TPC tumefarijika kwa PSSSF kutuletea mafunzo hayo muhimu, nina imani kuanzia sasa waandishi wetu watakuwa wanaandika habari za PSSSF kwa ufasaha, tunaomba mafunzo hayo yawe mlango wa kufungua ushirikiano chanya kwa pande zote” alifafanua Mwenyekiti huyo.


Kwa upande wake Mjumbe wa bodi ya Umoja wa Klabu za uandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bi. Salma Abdul alisisitiza ili waandishi wa habari na PSSSF iweze kufanikiwa kwenye utendaji kazi lazima kuwepo na ushirikiano bora, ili inapotokea changamoto kwa wananchi waandishi waweze kupata ushirikianao thabiti kwa kujibu maswali ya malalamiko na kuandika habari sahihi badala ya kuruhusu uvumi.


Afisa Mfawidhi wa PSSSF mkoani Tabora (TPC), Bi. Hanim Badiker akizumgumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkaoni Tabora. Kulia ni Mwenyekiti wa TPC, Bw. Juma Kapipi.

Akizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo Bi. Pendo Sallu ambaye ni mwanachama wa Tabora Press Club (TPC) kwanza amewashukuru PSSSF kwa semina hiyo akiwahakikisha kuwa watakwenda kuandika habari mbalimbali za kuelimisha na kuisaidia jamii juu ya masuala ya kiga ya jamii.

“Kwanza tunawashukuru PSSSF kwa semina hii, Tunawahakikishia kuwa tutakwenda kuandika habari mbalimbali za kuelimisha na kuisaidia jamii, Tunawaomba watumishi kutoka PSSSF wadumishe mawasiliano na ushirikiano hasa tunapokuwa tunataka ufafanuzi” alishauri Bi. Pendo Sallu.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa Uhusiano wa PSSSF  Bw. Abdul Njaidi, amesisitiza wajibu wa waandishi wa habari kuandaa vipindi na makala zinazotoa elimu ya kina kuhusu kinga ya jamii, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia wananchi kuondokana na malalamiko yanayotokana na ukosefu wa taarifa, na badala yake wataelewe vizuri sera, kanuni, mafao na faida tele zinazotolewa na Mfuko.


Afisa Uhusiano wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi akifafanua jambo katika semina hiyo
Ushirikiano kati ya PSSSF na waandishi wa habari wa Tabora unatarajiwa kuimarisha uwazi na kuleta matokeo chanya katika kufikisha taarifa sahihi kwa Watumishi wa Umma na wananchi kwa ujumla kwa kuondoa malalamiko na kujenga imani katika Mfuko.


Afisa wa PSSSF mkoani Tabora, Bw.Deogratius Kakoko akiwasilisha mada ya Ijue PSSSF kwenye kikao na waandishi wa mkoani Tabora.

No comments:

Post a Comment