ZIARA YA WIZARA YA MALIASILI YAANZA MOROGORO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, November 24, 2025

ZIARA YA WIZARA YA MALIASILI YAANZA MOROGORO



Na Mwandishi Wetu, MOROGORO


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Chande, wamewasili mkoani Morogoro na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi mkoani humo.

Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Kijaji na Mhe. Chande wanatarajiwa kutembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

Lengo la ziara hii ni kujifunza, kujionea shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii pamoja na kujitambulisha katika taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.


No comments:

Post a Comment