Na Mwandishi Wetu, Handeni TC
Madiwani wa Halmashauri ya Mji Handeni wameaswa kuzingatia miiko ya viongozi wa umma na kudumisha uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Baraza la Madiwani Desemba 4, 2025, kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji Handeni, Bakari Mussa kutoka Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma amewataka madiwani hao kuzingatia maadili, kuepuka mgongano wa maslahi, na kushirikiana kikamilifu na Mkurugenzi wa Halmashauri katika kusimamia shughuli za maendeleo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni, Maryam Ukwaju, amewahimiza madiwani kufanya kazi kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi na ya Halmashauri.
Amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji na kujiepusha na vitendo vinavyohatarisha uadilifu wa utumishi wa umma.

No comments:
Post a Comment