Magari ya huduma ya NMB yamefikia 15 kuchochea ujumuishaji wa kifedha - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, January 29, 2026

Magari ya huduma ya NMB yamefikia 15 kuchochea ujumuishaji wa kifedha


Magari yanayotoa huduma za kifedha ya Benki ya NMB, mahsusi kwa maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa matawi ya kawaida, sasa yamefikia jumla ya 15.

Ongezeko hili limekuja baada ya kuzinduliwa rasmi kwa magari mapya nane ya “Bank on Wheels”, ambayo ni matawi yanayotembea, yaliyobuniwa kuhakikisha huduma za benki zinawafikia wananchi moja kwa moja, iwe vijijini, sokoni au katika vituo vya biashara vya mbali.

Magari haya hayatoi tu huduma za kifedha, bali pia hutoa elimu ya kifedha, ufunguaji wa akaunti, huduma za mikopo, malipo na ushauri wa kibiashara kwa urahisi zaidi.

Uzinduzi wake unaashiria jitihada za NMB kuimarisha ujumuishaji wa kifedha nchini na kutekeleza mkakati wake wa kupeleka huduma za benki karibu na wananchi, huku akitumia teknolojia na mbinu bunifu kufanikisha maendeleo ya kiuchumi vijijini na kwenye jamii zisizo rasmi.

Kutambulishwa kwake kulikuwa sehemu ya unzinduzi wa Ajenda 2030 Jumatano wiki hii, ambayo ni Mpango Mkakati wa Kati wa NMB kwa kipindi cha 2026–2030, unaolenga pamoja na mambo mengine kupanua ujumuishaji wa kifedha nchini na kuharakisha ukuaji wa kijamii na kiuchumi.

Zoezi hilo lilisimamiwa na Msajili wa Hazina, Bw Nehemiah Mchechu, aliyeipongeza NMB kwa mchnago wake katika ujenzi wa taifa na kuboresha maisha ya Watazania kupitia masukuhisho bunifu na jumuishi.

Akizungumza kabla ya tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna, alisema kuwa magari haya yamebuniwa mahsusi kutoa huduma rasmi za kifedha moja kwa moja kwa jamii zisizo na matawi ya kawaida, ikiwemo vijiji vya mbali, sokoni na maeneo ya biashara kama minada.

“Haya siyo magari tu, ni milango ya fursa. Yanawawezesha wakulima, wafanyabiashara wadogo, wafugaji na wajasiriamali wadogo kupata huduma za akiba, mikopo, malipo na ushauri bila usumbufu wa kusafiri umbali mrefu au gharama kubwa,” Bi. Zaipuna alifafanua.

Kupitia huduma hii, mfanyabiashara hatumii siku nzima kusafiri kuweka fedha benki, na mkulima haasubiri siku ya soko ijayo kufungua akaunti. Badala yake, benki inafika moja kwa moja pale alipo kumhudumia.

Aidha, Bi. Zaipuna aliongeza kuwa utaratibu huu unaonesha imani thabiti ya NMB kwamba ujumuishaji wa kifedha lazima uende kwa wananchi, hasa kwa wale walioko kwenye sekta zisizo rasmi, ambao ndio msingi wa ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Huduma ya Bank on Wheels pia inasaifdia sana kutoa elimu ya kifedha na kuwajumuisha wananchi moja kwa moja katika mfumo rasmi wa kifedha.

Huduma hii imekuwa na mchango mkubwa katika kutekeleza mkakati wa NMB wa Village Banking ambao lengo lake kuu ni kizipeleka huduma za kifedha jijini.

Mkakati huu ni moja ya nguzo za msingi za Ajenda 2030 ambayo inalenga kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za kifedha, kuhamasisha ujasiriamali na kuharakisha mabadiliko ya kijamii na kiuchumi nchini.

Magari haya ya huduna yanawawezesha wananchi kufungua akaunti, kufanya miamala ya fedha, kukopa na kufanya usajili wa kidijitali.



No comments:

Post a Comment