"MILANGO IPO WAZI KWA UMIKIDO "WAZIRI MAKONDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, January 29, 2026

"MILANGO IPO WAZI KWA UMIKIDO "WAZIRI MAKONDA


Katika kuendelea kuimarisha umoja na kujitambulisha kwa Mamlaka mbalimbali, Mwenyekiti wa Umoja wa Vyombo vya Habari Mitandaoni Mkoa wa Dodoma (UMIKIDO), Benny Majata, amefanya mazungumzo mafupi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma leo Januari 29, 2026

Katika mazungumzo hayo, sambamba na kujitambulisha kwa Waziri Makonda, Majata amemweleza kuhusu malengo ya kuanzishwa kwa UMIKIDO, ikiwemo kusimamia maudhui yenye weledi, kuhamasisha maadili ya habari mtandaoni, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya vyombo vya habari na Serikali.

Kwa upande wake, Waziri Makonda amesema milango ya Wizara ipo wazi kwa UMIKIDO kufika ofisini kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kina juu ya namna Wizara itakavyoweza kusaidia umoja huo kutimiza malengo yake.

No comments:

Post a Comment