
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), amewasilisha taarifa ya utekelezaji ya Wizara katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Pili wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 19 Januari, 2026 Jijini Dodoma ambapo jumla ya taarifa 16 za utekelezaji wa majukumu ya Wizara na Taasisi zake zinatarajiwa kuwasilishwa mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Thimotheo Paul Mnzava (Mb)
Aidha, Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb.), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu Bw. Nkoba Mabula, Menejiment ya Wizara na Wakuu wa Taasisi na vyuo vilivyopo chini ya Wizara.







No comments:
Post a Comment