WIZARA YA NISHATI KUSHIRIKIANA NA TBC KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, January 15, 2026

WIZARA YA NISHATI KUSHIRIKIANA NA TBC KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Nishati, Bi. Neema Mbuja amepokea ujumbe rasmi kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wenye lengo la kuimarisha ushirikiano katika kuitangaza Wizara ya nishati hususani katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.

Akizungumza leo Januari 15, 2026 Katika ofisi za Wizara Mtumba Jijini Dodoma, baada ya kupokea ujumbe huo, Bi. Neema Mbuja alimshukuru Mkurugenzi wa Habari na Matukio Shirika la Utangazaji Tanzani (TBC), Bi. Eshe Muhidin pamoja na timu yake kwa kuendelea kuitangaza Wizara ya nishati pamoja na ajenda ya nishati safi ya kupikia kupitia Bongo FM na TBC kwa ujumla.

“Tunashukuru sana juhudi za TBC katika kuelimisha jamii kuhusu nishati safi ya kupikia, kwani kupitia ushirikiano huu tunakusudia kuifanya ajenda hii isambae kwa upana zaidi na kuwafikia wananchi wengi zaidi ili kutimiza azma ya Mhe. Rais ya Kuhakikisha ifikapo 2034 asilimia 80% ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia” alisema Bi. Mbuja
Ameongeza kuwa wizara itaendelea kushirikiana kwa karibu na vyombo vya habari katika kuhakikisha taarifa sahihi za Nishati zinawafikia wananchi kwa wakati.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Habari na Matukio Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Bi. Eshe Muhidin ameishukuru Wizara ya Nishati kwa ushirikiano wao wa karibu huku akibainisha kuwa TBC ni wadau wakubwa katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

“Tunaishukuru Wizara ya Nishati kwa ushirikiano wao, kwani TBC imekuwa mdau mkubwa katika kuhakikisha wananchi wanahamasishwa kutumia nishati safi ya kupikia hivyo tuibebe ajenda hii kwa ukubwa zaidi kwa maslahi mapana ya Taifa lengo likiwa ni kumsaidi Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuifikisha ajenda ya Pika Kijanja kwa wananchi alisema Bi.Muhidin.
Aidha Bi. Muhidin aliambatana na Mkurugenzi wa Huduma za Redio TBC, Bi. Anna Kwambaza, pamoja na Mkuu wa Bongo FM, Bi. Anastazia Willherick.

No comments:

Post a Comment