MKAGUZI WA POLISI KATA YA KIMANGA AWATAKA VIJANA KUWA WAZALENDO NA KUCHUKIA UHALIFU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, March 20, 2026

MKAGUZI WA POLISI KATA YA KIMANGA AWATAKA VIJANA KUWA WAZALENDO NA KUCHUKIA UHALIFU


Mkaguzi wa Polisi Kata ya Kimanga, Mkoani Dar es Salaam Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/INSP) Faharia Juma, amewataka vijana kuwa wazalendo, na kuendelea kujifunza masuala ya dini, na kushiriki kikamilifu katika kudumisha amani na utulivu na kuuchukia uhalifu.

Amebainisha hayo alipokutana na vijana wa kata hiyo, ambapo amesisitiza umuhimu wa vijana kuwa na nidhamu na kuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo vya uhalifu huku akisisitiza kuwa uhalifu hauna faida yoyote kwa mtu binafsi wala kwa jamii.

Aidha, ameongeza kuwa taifa linawategemea sana vijana katika ujenzi wa jamii bora, hivyo ni muhimu kwao kuwa mfano mzuri na kukemea vitendo vya uhalifu vinavyojitokeza katika maeneo yao.

Kwa upande mwingine, amewahimiza vijana kuendelea kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ili kusaidia kudhibiti uhalifu na kuimarisha usalama wa jamii.

No comments:

Post a Comment