OPERESHENI MAALUM YAANZA ARUSHA KUKABILI BODABODA ZENYE KELELE NA TAA KALI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, March 26, 2026

OPERESHENI MAALUM YAANZA ARUSHA KUKABILI BODABODA ZENYE KELELE NA TAA KALI


Katika kuhakikisha huduma ya usafiri inakuwa salama pamoja na kupunguza kero zitokanazo na bodaboda, Kamati ya Usalama wilaya ya Arusha imeanzisha operesheni maalum ikihusisha ukamataji wa pikipiki ambazo zimetajwa kuwa sababu ya kero izo ikiwemo zinazotoa kelele za milipuko pamoja zile zilizofungwa taa zenye mwanga mkali.

Akizungumza leo katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha, Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha Dkt. Jacob Julius Rombo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo pamoja na kupongeza uongozi wa bodaboda katika wilaya hiyo kwa kuungana na Jeshi la Polisi katika kudhibiti uhalifu, amewataka wale wote wanaoharibu mifumo ya pikipiki ikiwemo bomba la moshi na kufunga taa zenye mwanga mkali kuacha mara moja.

Dkt. Rombo ameendelea kufafanua kuwa uongozi wa wilaya unatambua na kuthamini kazi ya bodaboda, hivyo akasisitiza kazi hiyo ni muhimu na ni sawa na kazi nyingine hivyo inapaswa kufanywa kwa kuzingatia sheria na kanuni za maadili ya kazi bila kuwa kero kwa watumiaji wengine wa barabara.

Sambamba na hilo amelitaka Jeshi la Polisi wilayani humo, kuendelea kuchukua hatua za kisheria kwa wale wote watakaokaidi maelekezo hayo, kwani pikipiki hizo sio tu zimekuwa kero kwa wananchi, pia zinasababisha madhara hususani kwa wale wenye changamoto za kiafya.

Kwa upande wake Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Georgina Matagi amebainisha kuwa kwa kushirikiana na uongozi wa bodaboda wilayani humo, kwa kipindi cha miezi mitatu wamefanya operesheni maalum dhidi ya pikipiki hizo ambapo wamefanikiwa kukamata pikipiki 248 zilizofungwa taa zenye mwanga mkali na pikipiki 13 zinazotoa kelele zenye mlipuko.

Aidha, amesema kuwa pamoja na pikipiki hizo kuharibiwa mifumo mbalimbali, katika operesheni hiyo wamebaini kuwa nyingine zinafichwa namba za usajili na kuandika majina ya watu ili kuficha uhalisia kwakuwa nyingine zinatumika katika matukio ya uhalifu.

Pia, amewataka madereva bodaboda kuhakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani na wale wachache wanaofanya vitendo hivyo kuacha mara moja kwani operesheni hiyo ni endelevu na wataendelea kuchukua hatua kwa mujibu.

No comments:

Post a Comment