
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (kushoto), akipokea zawadi ya fremu ya 'Ayatul Kursiyu' iliyomo katika Quran Tukufu, kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (wapili kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Joyce Mapunjo) na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Fortunatus Mganga, wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na PSSSF kwa makundi mbalimbali mjini Unguja, Zanzibar Machi 17, 2026. Mhe. Mkuya alipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (Wapili kushoto), akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Makuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (Wakwanza kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Joyce Mapunjo (Wapili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo (Wakwanza kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10, Mkurugenzi wa Lift Life Foundation (LLF), Bi. Mtumwa Mohamed (Watatu kushoto), wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na PSSSF kwa makundi mbalimbali huko Zanzibar Machi 17, 2026.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (Wapili kushoto), akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Makuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (Wakwanza kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Joyce Mapunjo (Wapili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo (Wakwanza kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10, Katibu wa Chama cha Wenye Albinism Zanzibar (ZAAO) Bw. Mohamed Abdallah Mohamed, wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na PSSSF kwa makundi mbalimbali huko Zanzibar Machi 17, 2026.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (Wapili kushoto), akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Makuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (Wakwanza kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Joyce Mapunjo (Wapili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo (Wakwanza kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10, Katibu wa Chama cha Wasioona Zanzibar (ZANABA), Bw. Mohamed Mbarouk, wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na PSSSF kwa makundi mbalimbali huko Zanzibar Machi 17, 2026.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (Wapili kushoto), akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Makuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (Wakwanza kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Joyce Mapunjo (Wapili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo (Wakwanza kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10, Katibu wa Chama cha Wenye Albinism Zanzibar (ZAAO) Bw. Mohamed Abdallah Mohamed, wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na PSSSF kwa makundi mbalimbali huko Zanzibar Machi 17, 2026.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo (kushoto), akiwakaribisha wageni wake kwenye futari iliyoandaliwa na PSSSF kwa makundi mbalimbali mjini Unguja, Zanzibar Machi 17, 2026.
Na Mwandishi Wetu - Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umekuwa faraja kubwa kwa Wastaafu waliolitumikia taifa hili.
Mhe. Dkt. Mwinyi ameyasema hayo kupitia hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, katika hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na PSSSF kwa ajili ya makundi mbalimbali visiwani Zanzibar Machi 17, 2026.
“Nachukua fursa hii kuwapongeza PSSSF kwa kuendelea kuwahudumia wanachama wetu, hasa wastaafu, kwani siku hizi ikifika tarehe 25 ya kila mwezi wastaafu hupokea pensheni zao, hongereni sana na muendelee kufanya hivyo, kwa hakika mmekuwa faraja kubwa sana kwa wastaafu wetu,” alisema.
Aidha, Mhe. Dkt. Mwinhyi alisema,katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, binadamu tunakumbushwa kutenda mema.
“Nawashukuru kwa kuandaa futari hii ya pamoja lakini pia kwa msaada mliotoa kusaidia makundi mbalimbali hapa Zanzibar.” Alisema.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema Mwezi huu wa Ramadhani unafundisha umuhimu wa binadamu kuwa na subira, huruma na kusaidiana kwa wale wenye uhitaji katika jamii yetu jambo ambalo PSSSF wamelifanya leo hii.
“Kama Waziri ninayesimamia taasisi iliyoandaa futari hii, tutaendelea kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uwajibikaji ili kuendelea kuwatumikia wananchi kwa haki na usawa.” Alisisitiza Mhe. Sangu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo alisema, katika kipindi hiki ulimwengu mzima, Wakristo na Waislamu wako kwenye Mfungo na wanakumbushwa kufunga, kufanya ibada na kusaidia wenye uhitaji.
“PSSSF tuna Sera ya Corporate Social Investment-CSR, mbayo lengo lake ni kusaidia jamii katika maeneo ambayo yameaninishwa kwenye sera na kwa hapa Zanzibar tumetoa shilingi milioni 30 ambazo zimekwenda kwenye taasisi za Zanzibar National Association of the Blind, Life Lift Foundation na Zanzibar Albinism Organisation.” Alifafanua Bw. Magambo.

No comments:
Post a Comment