Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu yake huku ikiendelea kuvutia sekta binafsi na kusaidia uwekezaji wenye tija katika vyuo vikuu na kuongeza kuwa Serikali inahitaji wawekezaji zaidi ili kuimarisha maendeleo ya elimu nchini.
Akizungumza Machi 6, 2026 jijini Dar es Salaam baada ya kuzindua Bodi mpya ya TCU ya kipindi cha 2026/29, Prof. Mkenda amesisitiza umuhimu wa kusimamia kikamilifu sheria na kanuni ili kuhakikisha wahitimu wanakuwa mahiri na wenye ushindani katika soko la ajira.
Aidha, ameonya kuwa kutosimamia ubora wa elimu kunaweza kuathiri uwezo wa wahitimu kazini, hivyo TCU haina budi kuendelea kudhibiti viwango vya elimu kwa umakini.
Aidha, amesema kuwa Serikali inaendelea kuongeza miundombinu ya elimu ya juu kwa kujenga kampasi mpya 16 katika maeneo ya pembezoni ili kuongeza fursa kwa vijana.
Vilevile, ameitaka TCU kuboresha mifumo ya ajira katika vyuo vikuu ili kupata wakufunzi mahiri watakaoinua viwango vya elimu nchini.






No comments:
Post a Comment