
Wafanyakazi Wanawake wa Sekta ya Maji wamemtambua Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, kwa tuzo mahsusi kwa kuthamini mchango mkubwa anaotoa katika kuimarisha na kuendeleza hiyo sekta hiyo nchini.
Hafla hiyo fupi imefanyika leo katika Ofisi za Bonde la Wami-Ruvu mkoani Morogoro, wakati wa kufanya tathmini ya Siku ya Maji Duniani, huduma ambayo inawagusa kina mama wa Tanzania kwa ukubwa.
Akikabidhi tuzo kwa niaba ya wafanyakazi wanawake wa Sekta ya Maji, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Nyasa, Mhandisi Elice Engelbert, ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kutambua uongozi thabiti na mchango wa Katibu Mkuu Mhandisi Mwajuma katika kusimamia na kuhamasisha utendaji kazi wenye tija, unaojumuisha usawa wa kijinsia na kuleta matokeo chanya kwa wananchi.
Katibu Mkuu Mhandisi Mwajuma ametumia wasaa huo kushukuru kwa heshima hiyo na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kudumisha mshikamano, weledi na uwajibikaji katika Sekta ya Maji, na kuhikiza kuendelezwa kwa juhudi za pamoja katika kuhakikisha huduma ya maji safi na salama inawafikia wananchi wote kwa ufanisi zaidi.
Katibu Mkuu Mhandisi Mwajuma amewahi kuibuka kinara kama Mhandisi Mama Bora nchini Tanzania.


No comments:
Post a Comment