

Anthony Maliki , wa kwanza kushoto waliosimama akiwa na wanafunzi wenzake waliopata ufadhili wa kwenda kusoma nchini Afrika Kusini Chuo cha Johannesburg, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Barrick na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) , waliokaa wa kwanza kushoto , Meneja Rasilimali Watu wa Barrick nchini , Lumbu Kumbula, Meneja Mkazi wa Barrick nchini , Dkt Melkiory Ngido, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa William Anangisye na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Shule ya Madini na Jiolojia (SOMG) Profesa Elisante Mshiu.
****
“Nikiwa ni miongoni mwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Johanesburg nchini Afrika ya Kusini nikisomea fani ya uhandisi wa madini kwa ufadhili wa kampuni ya Barrick Tanzania najivunia kuwa katika programu hii ya kuwapatia mafunzo wataalamu wa sekta ya madini wa siku zijazo na ninaamini ina manufaa makubwa kwa Tanzania ambayo ni nchi yenye hazina kubwa ya madini ya aina mbalimbali” anasema Antony Godfrey Mariki.
Godfrey Mariki ni miongoni mwa wanafunzi watano wa mwaka wa kwanza kutoka shule ya Madini na Sayansi ya Miamba (SoMG) katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam walioshinda ufadhili (Scholarship) ya kampuni ya Barrick yenye ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals ambaye kwa sasa anasoma kozi ya uhandisi wa madini nchini Afrika ya Kusini.
Katika mahojiano yaliyofanyika karibuni kutokea nchini Afrika ya Kusini, Mariki amesema anayo furaha kuona yeye na wenzake wanaendelea vizuri katika masomo yao wakiwa wanapata msaada na ufuatiliaji wa karibu kutoka kwa mfadhili yaani kampuni ya Barrick na Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambapo walikuwa wanasoma hapo awali.
”Ufadhili huu tuliopata naamini sio wa kifedha tu bali ni fursa ya kipekee ya kujiendeleza kitaaluma kwa kupata elimu bora kutoka chuo bora barani Afrika ikizingatiwa kuwa Afrika ya Kusini imeendelea zaidi katika sekta ya madini zaidi ya hapo katika vipindi vya likizo Barrick imetupatia fursa ya kupata mafunzo ya vitendo kwenye migodi yake ili tuweze kupata maarifa zaidi”,amesema Mariki.
Kuhusiana na progamu hii Mariki anasema kuwa Barrick imeonyesha maono yake kwa kuwekeza kwenye elimu inaolenga kuboresha sekta ya madini nchini Tazania “Kupitia program hii ni dhahiri kwamba Barrick inaanda waaalamu wazawa kutoka Tanzania watakaoendeleza na usimamia sekta ya madini katika siku za mbele ili kuhakikisha inatoa mchango mkubwa kwa ukuaji wa uchumi wa nchi sambamba na kuwanufaisha Watanzania”,amesema.
Mariki ameongeza kuwa anafurahi kuona Barrick mbali na kutoa ufadhili huu pia imekuwa na programu mbalimbali za mafunzo zinazolenga kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta ya madini ikiwemo kuendesha semina za wanafunzi wanaosoma fani ya madini na utafii wa madini kwa kutumia wataalamu wa kampuni ambapo pia imekuwa ikitoa fursa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kupata mafunzo ya vitendo katika migodi yake ya North Mara na Bulyanhulu.
Akielezea historia yake fupi ya elimu amesema elimu ya msingi alisoma katika Shule ya Royal iliyopo mjini Moshi na alipomaliza alichaguliwa kujiunga na Seminari ya St,James nayo ipo mkoani Kilimanjaro baadaye masomo ya juu ya sekondari katika shule ya Kisimiri ambayo imemjenga zaidi katika safari ya kutimiza ndoto yake akaweza kupata vigezo vya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusomea kozi aliyoipenda ya uhandisi wa Madini.
Mariki anaamini kuwa mafanikio yoyote yanapatikana kwa kuwa na bidii katika jambo lolote ambalo mtu anafanya na kutoa wito kwa vijana wenzake nchini kuchangamkia fursa zinazojitokeza kuanzia kwenye masomo,kazi,biashara na shughuli nyinginezo zote."Mafanikio yoyote maishani yanahitaji kufanya kazi kwa bidii",amesisitiza.
Anasema wakati serikali ya Tanzania inakwenda kasi katika kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya madini,kunahitajiwa uwekezaji wenye mipango mikubwa utakaowezesha miradi mbalimbali ya kimkakati inayoendelea kuanzishwa kuwa endelevu na sio tu kuwekeza kwenye fedha na teknolojia bali kuwekeza pia katika kupata wataalamu wa kuendesha miradi kwa kipindi cha sasa na miaka ya mbele.
Ameendelea kueleza kuwa kuwa bila kufanya uwekezaji wenye mtazamo wa kujenga biashara endelevu kwa miaka mingi, kuna hatari ya biashara nyingi hususani katika sekta nyeti kama za madini,usafirishaji na mafuta kuendelea kutegemea wataalamu wa kigeni na watanzania kuachwa nyuma na kubaki kama watazamaji.
Anashauri kuwa kuna haja ya kuwapatia vijana wengi wa kitanzania fursa za kusoma fani zenye wataalamu wachache katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi sambamba na kuanzishwa Progamu mbalimbali za kuwanoa vijana wa kitanzania wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya ufundi kwa kuwapatia mafunzo ya vitendo kwa ajili ya kuwaanda kwendana na mabadiliko yanayotokea katika kila sekta na kushika nafasi za uongozi katika siku za usoni.
Akiongea kuhusu kupata nafasi ya Ufadhili wa Barrick kusomea taaluma ya madini nchini Afrika ya Kusini Mariki, anaeleza kuwa anajivunia kuwa miongoni mwa wanafunzi wachache waliochaguliwa kwa kuwa ushindani wa kuipata nafasi ulikuwa mkubwa sambamba na mchujo mkali uliofanywa na wataalamu mbalimbali ili kuhakikisha na kujiridhisha kuwa wanachukua watu wenye uwezo, makini na waliopo tayari kujifunza."Nina uhakika tutafanya vizuri na kupata kile kilicho bora na kukirudisha kwa taifa katika kutumikia watanzania wote kwa manufaa ya nchi ",amesisitiza.
Anasema moja ya ndoto kubwa aliyokuwa nayo katika maisha yake ni kufanya kazi katika kampuni kubwa na zenye mifumo mizuri ya kazi, jambo ambalo linaelekea kutimia kutokana na kampuni ya Barrick kutangaza pia fursa kuwapatia ajira pindi watakapomaliza elimu sambamba na kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa vitendo wakati wote watakapokuwa masomoni.
Kuhusu mambo yanayomvutia kutamani kufanya kazi katika kampuni ya Barrick amesema ni mengi mbali na kupata maslahi mazuri na utaalamu wa viwango vya kimataifa pia anavutiwa na jinsi inavyotekeleza mkakati wake endelevu wenye mtazamo wa kujenga jamii endelevu kwendana na utekelezaji wa malengo endelevu ya milenia ya umoja wa mataifa (MDGs).
"Inafurahisha kuona kampuni inayapa kipaumbele masuala ya msingi katika kujenga biashara endelevu kama vile utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji,usalama wa wafanyakazi wake ,kushirikiana na jamii zilizopo katika maeneo inakofanyia biashara zake kama ambavyo inafanya kazi na wazabuni wa ndani kuhakikisha inafanya manunuzi ya ndani ya nchini kwa asilimia kubwa ,kuendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wazabuni ili nao biashara zao zikuwe na kuwa endelevu bila kusahau kufanikisha miradi mbalimbali ya kusaidia jamii hususani katika sekta za elimu, ,afya, ,maji safi na salama na uboreshaji wa miundombinu ya barabara", amesema Samson.
Mariki, anaeleza kuwa anaamini kuwa hadi kufikia kuhitimu shahada yake ya kwanza nchini Afrika ya Kusini, atakuwa amejifunza mambo mengi yatakayomsaidia katika safari yake ndefu ya kuwa mtaalamu wa madini sambamba na kuwa mbunifu na kutoa mawazo ya kitaalamu yanayowezesha kukabili changamoto na kuwezesha sekta ya madini nchini Tanzania kusonga mbele kwa mafanikio makubwa.
Amemalizia kwa kutoa ushauri kwa wawekezaji wengine wanaotoka nje na ndani ya nchi kuiga mfano wa Barrick kwa kuwa na mtazamo wa kujenga biashara endelevu sambamba na kuwa na programu za kuandaa wataalamu wazawa kwa kuwawezesha kupata elimu na utaalamu kama ambavyo imedhamini wanafunzi watano kusomea utaalamu wa fani ya madini nje ya nchi.
"Programu kama hii ni muhimu kwa kuwanoa vijana wasomi kupata ujuzi wa viwango vya kimataifa ,natamani kuona pia idadi ya vijana wanaochukuliwa katika Programu hii kuongezwa zaidi ya sasa ili inufaishe vijana wengi wa kitanzania", amesisitiza.


No comments:
Post a Comment