Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Ikungi Mashariki, Miraji Mtaturu, amefika Hospitali ya Wilaya ya Ikungi kumjulia hali mke wa Katibu wake, Ally Juma Rehani, ambaye amelazwa akipatiwa matibabu.
Mtaturu ametumia fursa hiyo kumtakia mgonjwa huyo uponyaji wa haraka ili aweze kurejea katika majukumu yake ya kila siku ya kuihudumia familia yake.
Aidha, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais, Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya Hospitali ya Wilaya ya Ikungi, ambayo kwa sasa inatoa huduma mbalimbali ikiwemo upasuaji mkubwa na mdogo, hali inayochangia kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Pia amewatakia wananchi wa Ikungi na Watanzania wote kwa ujumla Sikukuu njema ya Pasaka.







No comments:
Post a Comment