WATU WENYE ULEMAVU JIMBO LA MTUMBA KUWEZESHWA NA MIRADI YA KIUCHUMI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, April 4, 2026

WATU WENYE ULEMAVU JIMBO LA MTUMBA KUWEZESHWA NA MIRADI YA KIUCHUMI


Na Mwandishi Wetu - Dodoma


Wananchi wenye ulemavu wa Jimbo la Mtumba kupitia programu mbalimbali za uwezeshwaji wananchi kiuchumi na na mikopo ya serikali kuwezeshwa miradi ya kiuchumi ili waweze kujitegemea na kujiendeleza kiuchumi.

Hayo yamesemwa leo na Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya usaidizi kwa watu wenye ulemavu wa Jimbo la Mtumba.

“Tunamshukuru Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuwajali na kuwaendeleza watu wenye ulemavu nchini.

Suala la mikopo na uwezeshwaji kiuchumi watu wenye ulemavu ni ukombozi mkubwa katika kuwafanya waweze kujitegemea.

Jimbo la Mtumba tumeandaa programu mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kiuchumi”Alisema Mavunde

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye Ulemavu(SHIVYAWATA) Mkoa wa Dodoma Ndg. Omar Lubuva ameishukuru serikali kwa namna ambavyo imekuwa mstari wa mbele kutatua changamoto za watu wenye ulemavu,pia amemshukuru Mbunge Mavunde kwa msaada wa viti mwendo na fimbo nyeupe kwa watu wenye ulemavu kwa kuwa hiyo ni hatua kubwa katika kupunguza changamoto za watu wenye ulemavu.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma,Ndg. Sakina Mbugi amesema serikali itaendelea kuwa bega kwa bega na watu wenye ulemavu katika utatuzi wa changamoto zao pamoja na kuendelea kuongeza fursa za kiuchumi kwa kundi hili.




No comments:

Post a Comment