NAIBU WAZIRI KASEKENYA AMPONGEZA MKANDARASI UJENZI WA DARAJA LA LUBANGALALA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, April 13, 2026

NAIBU WAZIRI KASEKENYA AMPONGEZA MKANDARASI UJENZI WA DARAJA LA LUBANGALALA


Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng.Godfrey Kasekenya amempongeza mkandarasi Aweasome Co. Ltd aliejenga daraja la dharura kwa muda mfupi katika mto Lubangalala Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Akizungumza alipokagua daraja hilo Eng. Kasekenya amewataka wakandarasi kufanyakazi kwa bidii na ubunifu hususan katika mazingira ya dharura ili kuwapunguzia wananchi kero pale uharibifu wa miundombinu ya barabara na madaraja unapotokea.

"Nakupongeza mhandisi Grace Frederick kwa kazi nzuri na ya kizalendo ulioifanya katika kutafuta ufumbuzi wa haraka na kurudisha mawasiliano kati ya wananchi wa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya na Ileje mkoani Songwe tunataka wakandarasi kama ninyi", amesema Eng. Kasekenya.

Naibu Waziri huyo wa Ujenzi amempongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kibali cha kurejesha huduma za mawasiliano katika eneo hilo mara baada ya daraja kubomoka kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

"Kurejea kwa mawasiliano kati ya wilaya za Rungwe na Ileje kutawawezesha wananchi wa mikoa ya Mbeya na Songwe kuendelea na shughuli za kijamii na kiuchumi na hivyo kujiletea maendeleo", amesisitiza Eng. Kasekenya.

Daraja la Lubangalala linalounganisha mkoa wa Mbeya na Songwe lilisombwa na mafuriko yaliyotokea wakati wa maporomoko Machi 25 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 22 na majeruhi kadhaa.

Akizungunza kwa ufupi mkandarasi huyo wa kampuni ya Awesome Co Ltd, Grace ameshukuru kwa kuaminiwa na kupewa ushirikiano tangu Machi 27 alipoanza Ujenzi huo

Mmoja wa wananchi Rungwe Emeria Haonga amesema mafuriko yaliyotokea yamewaacha na majanga kwani licha ya kukata mawasiliano yameharibu mazao na hivyo ameishukuru Serikali kwa kuchukua hatua haraka.








No comments:

Post a Comment