REA YANADI MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KUSAMBAZA NISHATI VIJIJINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, April 2, 2026

REA YANADI MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KUSAMBAZA NISHATI VIJIJINI


Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeshiriki katika mahojiano maalum kujadili mafanikio na hatua za ujenzi wa Miradi ya Kusambaza Nishati maeneo ya Vijijini yaliyorushwa Mubashara kupitia Luninga ya ITV.

Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka REA, Mha. Jones Olotu na Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala, Mha. Advera Mwijage wameshiriki katika mahojiano hayo Machi 2, 2026 Jijini Dar es Salaam ambapo walieleza bayana mafanikio na hatua mbalimbali zilizofikiwa za ujenzi wa Miradi ya Kusambaza Nishati Vijijini.


Awali akizungumza katika mahojiano hayo, Mha. Olotu amesema baada ya kuridhishwa na mafanikio ya REA, Serikali iliiongeza fedha na hivyo kuiwezesha kutanua wigo wa Miradi.

"Hadi sasa tumekamilisha Usambazaji umeme kwenye vijiji na tunaendelea na vitongoji. Tulianza na vijiji 506 na tukianza na maeneo ya kipaumbele ya Serikali ambayo yanatoa huduma ya moja kwa moja kwa wananchi ikiwemo makao makuu ya Wilaya, shule, vituo vya afya, visima vya maji," amesema Mha. Olotu.


Kwa upande wake Mha. Advera alisema REA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya Nishati Safi ya Kupikia ili kutimiza dhamira ya Serikali ya asilimia 80 ya wananchi wawe wanaotumia Nishati Safi ya Kupikia ifikapo Mwaka 2034.

Mha. Advera alizungumzia namna ambavyo REA inawezesha miradi mbalimbali ikiwemo ya kuzalisha umeme kwa Nishati ya maji na jua.

"Kwa sasa hivi tunayo miradi mingi inayoendelea kwenye upande wa ujenzi wa gridi ndogo, tumekwishajenga zaidi ya gridi ndogo 70. Zinatumia Nishati ya maji na Nishati ya jua," amesema. 

Amesema kuwa REA vilevile inawezesha wananchi maeneo ya visiwani kupata Nishati ya Umeme kwa lengo la kujiletea maendeleo.

"Tunao Mradi mkubwa ambao unatekelezwa katika visiwa na tunafunga mifumo 20,000 ya Umeme jua kwa hatua za awali kwa bei ya ruzuku: tumemjali Kila mwananchi kupata Nishati hiyo kulingana na kipato chake," amesema Mha. Advera.

Mahojiano hayo yalitoa fursa kwa Jukwaa la Wahariri (TEF) na wananchi kuuliza maswali, kutoa maono na kupongeza hatua zilizofikiwa.

No comments:

Post a Comment