WANANCHI WASISITIZWA MALEZI BORA KUPATA VIONGOZI WANAO CHUKIA RUSHWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, April 15, 2026

WANANCHI WASISITIZWA MALEZI BORA KUPATA VIONGOZI WANAO CHUKIA RUSHWA


Wananchi wa kata ya kisangura Wilaya Serengeti Mkoa wa Mara wamesisitizwa kuendelea kutoa malezi bora kwa watoto ili kupata jamii yenye hofu ya Mungu na yenye kuchukia uhalifu na vitendo vya Rushwa.

Hayo yamebainishwa na Mkaguzi kata ya Kisangura Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Mkaguzi wa Polisi (INSP) Genuine Kimario wakati akitoa elimu hiyo kwa wananchi wa familia moja katika kata hiyo.

Ameongeza kuwa ili jamii iendelee kuwa na maadili inategemea msingi mzuri wa malezi yanayoanzia katika familia ambapo amesisitiza dhamira hiyo. 

No comments:

Post a Comment