WAZIRI GWAJIMA ATAKA MWONGOZO WA NDOA KUDHIBITI WATOTO WA MITAANI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, April 1, 2026

WAZIRI GWAJIMA ATAKA MWONGOZO WA NDOA KUDHIBITI WATOTO WA MITAANI



Na Okuly Julius, OKULY BLOG, DODOMA



Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima, amewataka maafisa ustawi wa jamii kushirikiana na wanandoa waliodumu kwa muda mrefu kuandaa muongozo utakaobainisha changamoto za ndoa na mbinu za kuzitatua, kwa lengo la kupunguza migogoro katika ndoa changa inayochangia ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.

Dkt. Gwajima ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto Anayeishi na Kufanya Kazi Mtaani yatakayofanyika Aprili 12 mwaka huu. 


Amesema migogoro ya kifamilia ni miongoni mwa sababu kuu zinazochangia watoto kuishi mitaani.

Aidha, ameelekeza mikoa yote nchini kuanza mara moja zoezi la kuwaokoa watoto hao kwa kuwafikia katika maeneo wanayofanyia shughuli zao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri, akiwasilisha takwimu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, amesema Katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2024 hadi 2026, jumla ya watoto 326 wameokolewa katika mkoa wa Dodoma. Mwaka 2024 waliokolewa watoto 122, wakiwemo 33 kutoka Bahi, 49 Dodoma Jiji na 40 Kongwa, huku 99 wakiunganishwa na familia zao. Mwaka 2025, watoto 135 waliokolewa—35 kutoka Bahi, 22 Dodoma Jiji na 78 Kongwa—ambapo 125 waliunganishwa na familia zao. Kwa mwaka 2026 hadi sasa, watoto 69 wameokolewa, wakiwemo 43 kutoka Bahi, 10 Dodoma Jiji na 16 Kongwa, huku 65 tayari wameunganishwa na familia zao.

Maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika katika kila mkoa yakiongozwa na kaulimbiu isemayo, “Malezi na Ulinzi wa Mtoto; Wajibu Wetu Sote.”

No comments:

Post a Comment