WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA BELARUS AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 28, 2026

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA BELARUS AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI


Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Belarus, Mheshimiwa Maxim Ryzhenkov, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia Aprili 28 hadi 30, 2026, kufuatia mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo.

Mheshimiwa Ryzhenkov amewasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ambapo alipokewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe, pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Belarus nchini Mhe.Dzmitry Krasouski.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Ryzhenkov anatarajiwa kufanya mazungumzo ya pande mbili na mwenyeji wake, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Aprili 28, 2026, jijini Dar es Salaam. Aidha, atakutana na viongozi wengine wa Serikali kwa lengo la kuendeleza na kupanua ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Belarus pamoja na kukuza ushirikiano wa kiuchumi katika maeneo yenye maslahi ya pamoja.







No comments:

Post a Comment