
Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) inatarajia kutekeleza Mradi wa Matumizi Bora ya Nishati katika Jengo la Wizara ya Nishati na baadaye Mji wote wa Serikali Mtumba.
Hayo yameelezwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga wakati akizungumza katika kikao cha kujadili Utekelezaji wa mradi huo na Meneja Miradi wa UNDP, Aaron Cunningham tarehe 1 Aprili, 2026 katika Mji wa serikali Mtumba, Dodoma.
Mhandisi Luoga amesema mradi wa Matumizi Bora ya Nishati utatekelezwa kwa kuanzia katika jengo la Wizara ya Nishati kwa kufunga mitambo midogo ya kuzalisha umeme kwa kutumia Jua, upepo na Miundombinu yenye kutumia umeme kidogo na kwa ufanisi na hivyo kuwezesha Jengo hilo kuwa na umeme safi na wa uhakika.
Vilevile, mradi huo utahusisha pia kufunga mashine za kuchajia magari ya umeme katika viwanja vya jengo hilo na maeneo ya maegesho ya magari.
“ Tutatekeleza mradi huu kwa kuanzia na jengo la Wizara kwakuwa ndiyo wenye dhamana ya kusimamia Sekta ya Nishati ili iwe mfano kwa Taasisi zingine za Serikali na Binafsi, baadaye mradi huu utatekelezwa katika mji wote wa serikali hapa Mtumba. Hii itasaidia kupunguza gharama za kutumia umeme katika majengo hayo na kuwezesha upatikanaji umeme wa uhakika”, alisema Mhandisi Luoga
Kwa upande wake, Meneja Miradi wa UNDP, Aaron Cunningham, amesema UNDP iko tayari kushirikiana na Wizara ya Nishati kutekeleza mradi huo kwa kuwa tayari wamekuwa wakishirikiana katika miradi mbalimbali na inayoleta tija katika jamii na taifa kwa jumla.
Mradi huo utakuwa na ufanisi mkubwa kwa katika kupunguza gharama za umeme katika taasisi za serikali.
Ametaja baadhi ya miradi ambayo wameshirikiana na Wizara kuwa ni pamoja na mradi wa Matumizi bora ya Nishati ambapo Mkakati wake wa Miaka 10 ulizinduliwa Desemba, 2024




No comments:
Post a Comment