
Mbunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga (CCM) amepongeza hatua ya Wizara ya Nishati kupunguza utegemezi wa fedha kutoka nje katika utekelezaji wa miradi ya sekta ya nishati.
Akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya.Nishati na Taasisi zake kwa mwaka 2026/27, Silanga amesema hatua hiyo inatoa uhakika wa utekelezaji wa miradi ya nishati ambayo ni mhimili mkuu katika ukuaji wa uchumi.
Wizara ya Nishati imeomba kuidhinishiwa Sh trilioni 2.53 kwa ajili ya matumizi ya wizara na taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2026/27, kati ya fedha hizo, Sh trilioni 2.46 sawa na asilimia 97.5 ya bajeti yote ya wizara zimeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
Kati ya fedha za maendeleo zilizoombwa, Sh trilioni 1.6 ni fedha za ndani, huku Sh bilioni 859.92 zikiwa fedha za nje.

No comments:
Post a Comment