Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameipongeza Timu ya Taifa ya Wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite Queens U-20, kwa kufuzu Kombe la Dunia la Wasichana U-20 litakalofanyika nchini Poland mwezi Septemba mwaka huu.
Mhe. Dkt. Mwinyi amesema ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Timu ya Taifa ya Cameroon katika mchezo uliochezwa leo tarehe 10 Mei, 2026 katika Uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar, umeonesha kiwango kikubwa cha uzalendo, nidhamu na juhudi za vijana wa Tanzania katika kuipeperusha vyema bendera ya Taifa kimataifa.
Amesema mafanikio hayo ni hatua kubwa kwa maendeleo ya soka la wanawake nchini na yameleta heshima kwa Taifa lote, huku akiwasisitiza wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu kuendelea kufanya maandalizi mazuri kuelekea mashindano hayo ya dunia.
Aidha, Mhe. Rais Dkt. Mwinyi amewapongeza mashabiki na Watanzania wote kwa kuendelea kutoa hamasa kubwa kwa timu hiyo katika safari yake ya mafanikio.
“Kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Wananchi wa Zanzibar nawapongeza Tanzanite Queens U-20 kwa mafanikio haya makubwa ya kihistoria.
Mmeonyesha uwezo, uzalendo na moyo wa kupambana kwa ajili ya Taifa letu,” amesema Mhe. Dkt. Mwinyi.

No comments:
Post a Comment