Na Okuly Julius, OKULY BLOG
Serikali imeendelea kuimarisha usalama wa usafiri majini nchini kupitia usimamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), ambapo idadi ya watoa huduma waliopatiwa leseni imeongezeka hadi 1,794 katika kipindi cha Julai 2025 hadi Machi 2026.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma.
Ambapo amesema, idadi hiyo imeongezeka kutoka watoa huduma 1,556 waliokuwa wamesajiliwa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2024/25, ikiwa ni ishara ya kuongezeka kwa udhibiti na uboreshaji wa sekta ya usafiri majini.
Amesema Serikali kupitia TASAC imeendelea kusimamia usalama wa vyombo vya usafiri majini, kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaotokana na shughuli za meli, pamoja na kutoa huduma za ugomboaji na uondoshaji wa shehena kwa bidhaa mbalimbali nchini.
Katika hatua nyingine, Serikali imeeleza mafanikio katika kuimarisha usalama wa usafiri katika Ziwa Victoria kupitia ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, ambapo mradi wa kikanda wa kuboresha mawasiliano na uchukuzi unaendelea kutekelezwa.
Mradi huo umehusisha ujenzi wa Kituo Kikuu cha Uratibu wa Utafutaji na Uokoaji pamoja na ununuzi wa boti mbili za utafutaji na uokoaji na boti moja ya matibabu (Ambulance Boat), ambazo tayari zimeanza kutoa huduma katika Ziwa Victoria.
Aidha, Profesa Mbarawa amesema, serikali imenunua boti nyingine mbili za kisasa za utafutaji na uokoaji ambazo zimeanza kufanya kazi katika Ziwa Tanganyika pamoja na eneo la Bahari ya Hindi katika Mkoa wa Tanga, hatua inayolenga kuimarisha uokoaji na kupunguza ajali za majini.
Profesa Mbarawa amesema hatua hizo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuhakikisha usafiri majini unakuwa salama, wa kisasa na wenye ufanisi zaidi katika kulinda maisha ya wananchi na kukuza biashara za majini nchini.

No comments:
Post a Comment