Wanafunzi wa shule ya msingi Nzuguni Jijini Dodoma wametoa wito wazazi, walezi pamoja na walimu kuweka mahusiano mazuri na wanafunzi hao ili waweze kufikisha taarifa za vitendo vya ukatili wanavyo kumbana navyo majumbani na shuleni.
Hayo yamejiri Mei 20, 2026 wakati wakipewa elimu ya ushirikishwaji wa jamii na elimu ya ukatili na watendaji wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma walipofika shuleni hapo kutoa elimu ya kuwaongezea uelewa pamoja na kutoa taarifa juu ya vitendo viovu.
Akizungumza na wanafunzi hao, Mkuu wa Ushirikishwaji wa Jamii wilaya ya Dodoma Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Regina Mtana amewasihi wanafunzi hao kutokufumbia macho vitendo vya ukatili ikiwemo ubakaji na ulawiti ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakivitenda vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na sheria.
Vilevile, ASP Mtana amewataka wanafunzi hao kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu na kueleza jinsi Jeshi la Polisi lilivyo jipanga kuhakikisha vitendo hivyo vinafikia ukomo kupitia mfumo wa upokeaji taarifa kwa siri na kuzifanyia kazi kwa mujibu wa sheria na kuwafikisha wahusika mahakamani pindi upelelezi unapo kamilika.
"Tunadawati la jinsia mahususi kwaajili ya kupokea taarifa za ukatili wa jinsia zote kila mwanawafunzi anawajibu wa kukemea vitendo hivyo toeni taarifa hata kwanjia ya siri tutazifanyia kazi si ukatili tu hata taarifa za uhalifu mwengine wizi, uvunjaji pamoja wauza dawa za kulevya jamii inawajibu kukemea vitendo hivyo na sisi Jeshi la Polisi tutawawajibisha kwa mujibu wa sheria" alisema ASP. Mtana
Kwa upande wa wanafunzi wa shule hiyo wamefanya majadiliano ya pamoja na Jeshi la Polisi na kuweka mikakati ya pamoja ya kuzuia ukatili dhidi ya wanafunzi pamoja na jamii inayowazunguka ambapo moja ya mikakati hiyo ni kuwa mabalozi wa kupinga vitendo viovu na kuviripoti kwa Jeshi la Polisi ili viweze kuchukuliwa hatua.
Pia, uongozi wa Shule hiyo wamepongeza mikakati ya Jeshi la Polisi kwa kusogeza huduma kwa wananchi pamoja na kutembelea shuleni hapo na kutoa elimu itakayo saidia kupunguza vitendo viovu sambamba na kushirikiana na Polisi kata wa Kata ya Nzuguni Mkaguzi wa Polisi INSP. shekhdafa






No comments:
Post a Comment