WATAALAMU KWENYE MAFUNZO YA KUKABILIANA NA MAAFA WATAKIWA KUYATUMIA KUKABILIANA NA MAAFA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 1, 2026

WATAALAMU KWENYE MAFUNZO YA KUKABILIANA NA MAAFA WATAKIWA KUYATUMIA KUKABILIANA NA MAAFA.






Na Mwandishi wetu- Dodoma

Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Hosea Ndagala amewataka wataalamu ambao wamepatiwa mafunzo ya kukabiliana na maafa kuyatumia vyema katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na kurejesha hali baada ya maafa.

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo ya siku nne ya kujiandaa na kukabiliana na maafa kwa Kamati ya wataalamu , Timu ya kukabiliana na maafa na watumishi wa Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya dharura (REOCC) Mkoa wa Dodoma.



Brigedia Jenerali Ndagala ameeleza kuwa Awamu ya kwanza ya utekelezaji ilianza katika Mkoa wa Mwanza na Arusha, ambapo hatua za kuanzisha Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura pamoja na kuimarisha Timu ya kukabiliana na Maafa ilianza kutekelezwa Mikoay a Mwanza na Arusha huku akiongeza kuwa mafunzo hayo yataendelea katika Mikoa yote Nchini.


Sambamba na hilo amebainisha kuwa mafunzo hayo ni nyenzo muhimu katika kujenga na kuimarisha uwezo wa kitaalamu na kiutendaji kwa watumishi wanaohusika na uendeshaji wa kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura.

Pia ameeleza kuwa Uanzishwaji wa kituo hicho katika Mkoa wa Dodoma ni hatua muhimu kwani kitawezeshaufuatiliaji wa matukio kwa ukaribu, ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa kwa wakati, pamoja na kuimarisha mawasiliano kati ya wadau mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Dodoma na Taifa kwa ujumla ili kuokoa maisha ya watu na mali zao.

Aidha Brigedia Jenerali Ndagala amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule kwa kukubali mafunzo hayo kutolewa katika timu hizo na kuanzisha Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura cha Mkoa ambacho kitaunganishwa na Kituo cha Taifa akisema uamuzi huo unaonyesha dhamira thabiti ya uongozi wa Mkoa wa kuimarisha utayari, mwitikio wa haraka na uratibu madhubuti wakati wa dharura.



No comments:

Post a Comment