DODOMA YANG’ARA, HATUA YA MAKUNDI SOKA WASICHANA UMITASHUMTA 2026 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, June 10, 2026

DODOMA YANG’ARA, HATUA YA MAKUNDI SOKA WASICHANA UMITASHUMTA 2026


Na OWM-TAMISEMI,Iringa


Mashindano ya soka kwa wasichana katika Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) 2026 yameendelea kupamba moto huku timu mbalimbali zikionesha ushindani mkubwa katika michezo inayofanyika kitaifa mkoani Iringa.

Katika michezo iliyochezwa leo, Juni 10, 2026, kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Lugalo, timu ya Mkoa wa Dodoma ilionyesha kiwango cha juu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji Iringa.

Katika mchezo mwingine, Katavi iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Simiyu, huku Morogoro ikiendeleza matokeo mazuri kwa kuifunga Shinyanga mabao 2-0. Nayo Mwanza iliendelea kufanya vyema baada ya kuichapa Kigoma mabao 2-0.

Mashindano hayo ambayo bado yako katika hatua ya makundi yameendelea kushuhudia ushindani mkali, huku timu nyingi zikionesha maendeleo makubwa na kiwango cha juu cha mchezo ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Mbali na soka la wasichana, michezo mingine iliyoendelea asubuhi ya Juni 10, 2026 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Lugalo ni pamoja na mpira wa kikapu kwa wasichana na wavulana, kriketi pamoja na goalball.

UMITASHUMTA 2026 inaendelea kuwa jukwaa muhimu la kuibua na kukuza vipaji vya michezo kwa wanafunzi wa shule za msingi kutoka mikoa mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment