Kamishna msaidizi kanda ya kati wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya ,Joseph kisusi amesema serikali inaendelea na jitihada za kupiga vita dawa za kulevya kwa kuchukuwa hatuwa za oparesheni na uelimishaji ili kujenga ustawi wa jamii.
ameyasema hayo wakati akiwasilisha wasilisho la hali ya dawa za kulevya kanda ya kati kwa kipindi cha julai 2025 hadi juni 2026 katika maadhimisho ya siku ya kilele cha kupinga vita matumizi ya dawa za kulevya duniani yaliyofanyika viwanja vya ST. JOHN vilivyopo Jijini Dodoma juni 26,2026 ambapo maadhimisho hayo yaliambatana na ufanyaji usafi hosipitali ya taifa ya afya ya akili mirembe , michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu na kuvuta kamba.
hata hivyo amesema kuwa zipo takwimu mbalimbali zinazo onesha makundi ya watu wanao tumia madawa hayo na kuathirika pamoja na takwimu za kukamatwa kwa dawa za kulevya na mashamba ya bangi kanda kati ambayo ni mikoa ya Dodoma ,Morogoro na Singida.
"Kundi rika ambalo limeathirika zaidi na madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ni vijana kuanzia miaka 16 mpaka miaka 44 na kwa kipindi cha julai 2025 hadi juni 2026 jumla ya watuhumiwa 242 wa makosa ya dawa za kulevya walikamatwa na jumla ya kesi 173 zilifunguliwa ambapo kesi hizo baadhi ya watuhumiwa walihukumiwa kutumikia adhabu na wengine kuachiwa huru kwa mujibu wa sheria.
"Mkoa wa Dodoma wilaya ya Bahi tumekamata kilo za 25 mirungi kilo 0 heroni kilo 0 mashamba ya bangi 0 ,wilaya ya Dodoma mjini bangi kilo 349.73 mirungi kilo 234 heroni kilo 0.462 mashamba 0 ,Wilaya ya chamwino bangi kilo 120.68 mirungi kilo 98 heroni 0 mashamba ya bangi 15 ,Wilaya ya mpwapwa bangi kilo 40 mirungi kilo 0 heroni kilk 0 mashamba ya bangi 0 ,Wilaya ya Kongwa bangi kilo 140 mirungi kilo 0 heroni kilo 0 mashamba ya bangi 0 wilaya ya Kondoa bangi kilo kilo 485 mirungi kilo 204 heroni kilo 0 mashamba ya bangi 21 na wilaya ya chemba bangi kilo 0 mirungi kilo 0 heroni kilo 0 mashamba ya bangi 0.
"Mkoa wa Morogoro wilaya ya morogoro mjini tumekamata kilo za bangi 500 mirungi kilo 0 heroni 0.25 mashamba 0 Wilaya morogoro vijijini kilo za bangi 234 mirungi kilo 0 heroni kilo 0 mashamba 0 Wilaya ya mvomero kilo za bangi 20804.45 mirungi 0 heroni 0 mashamba 1445 Mkoa wa singida wilaya ya singida mjini tumekamata kilo za bangi 35 mirungi kilo 0.34 heroni kilo 0 mashamba 0,"alisema kisusi.
Aliongeza kuwa ongezeko kubwa la waathirika wa uraibu wa pombe nchini linaongozwa na watumishi wa umma na wanafunzi ambapo bohari kuu ya dawa (msd ) imeagiza dawa saidizi ambayo itasaidia kuacha pombe na dawa hiyo inatarajia kuingia ndani ya mwaka huu.
"Waraibu wa aina nyingine ya dawa za kulevya kama vile pombe ,sigara valium ongezeko limekuwa kubwa ,matumizi haya ya dawa za kulevya yanaambatana na magonjwa mbalimbali yakiwemo yakimwili kama vile UKIMWI ,Homa ya ini ,Kifua kikuu na Magonjwa ya akili hivyo mnapaswa kuacha kabisa kutumia madawa.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Sakina Mbugi, amesema kuna umuhimu wa kuongeza elimu na ushiriki wa jamii katika kuwalinda vijana dhidi ya janga hilo.
Nao baadhi ya vijana wamesema ushawishi kutoka kwa marafiki na makundi wanayojiunga nayo umekuwa miongoni mwa sababu zinazowasukuma kuanza kutumia dawa.
Aidha Maadhimisho ya mwaka huu yanabeba ujumbe kwamba mapambano dhidi ya dawa za kulevya si jukumu la Serikali pekee, bali ni wajibu wa kila mmoja katika kulinda ndoto za vijana na mustakabali wa taifa.











No comments:
Post a Comment