SHEREHE ZA WIKI YA WAZAZI KITAIFA ZAOTA MBAWA HADI ITAKAPO TANGAZWA TENA WAKATI MWINGINE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 27, 2026

SHEREHE ZA WIKI YA WAZAZI KITAIFA ZAOTA MBAWA HADI ITAKAPO TANGAZWA TENA WAKATI MWINGINE

Na Boniphace -John Dodoma. 


Mwenyekiti  Taifa  Jumuiya ya Wazazi CCM, Maganya Abdul  Rajabu, ametangaza kuahirishwa kwa sherehe za Wiki ya Wazazi Kitaifa 2026 ambazo zilikuwa zikitarajiwa kufanyika mkoani Mwanza kuanzia Juni 30 hadi Julai 4, 2026.


‎ameyasema hayo   jijini Dodoma leo hii Juni 27, Maganya amesema uamuzi huo umejitokeza  kufuatia tamko la Serikali lililotolewa jana bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuhusu kusitishwa kwa mikutano yote ya hadhara inayofanywa na vyama vya siasa.


‎ameongeza kuwa maadhimisho hayo yalikuwa yafanyike chini ya kaulimbiu isemayo, "Malezi Bora na Uzalendo ni Msingi wa Taifa," huku yalitarajiwa kuwakutanisha wanachama na wadau mbalimbali kutoka maeneo tofauti tofauti ya nchi.


‎ameeleza  maandalizi ya maadhimisho hayo yalikuwa tayari yamekamilika katika ngazi za matawi, wilaya na mikoa, ambapo hatua iliyokuwa imebaki ilikuwa ni kukamilisha shughuli hizo katika ngazi ya kitaifa .


‎Amesisitiza kuwa kutokana na mazingira yaliyopo na maelekezo yaliyotolewa na Serikali, Jumuiya ya Wazazi imeamua kuahirisha sherehe hizo kwa muda usiojulikana hadi itakapotoa taarifa nyingine kuhusu tarehe mpya ya sherehe.


‎Aidha, amewataka wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM pamoja na wananchi kwa ujumla kupokea uamuzi huo kwa utulivu na kuendelea kufuatilia taarifa rasmi zitakazotolewa na uongozi wa jumuiya kuhusu hatua zitakazofuata.


‎Hata hivyo,Maganya ameomba radhi kwa wanachama, wadau na wananchi wote hasa waliokua wameanza safari ya kuelekea jijini mwanza kutokana na usumbufu uliojitokeza kufuatia kuahirishwa kwa maadhimisho , akiahidi kuwa taarifa mpya itatolewa mara baada ya mazingira kuruhusu shughuli hizo kufanyika.

No comments:

Post a Comment