MASHINDANO YA UJUZI YA WORLD SKILLS TANZANIA 2026 YAANZA TANGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, August 20, 2026

MASHINDANO YA UJUZI YA WORLD SKILLS TANZANIA 2026 YAANZA TANGA

Mashindano ya Kitaifa ya Ujuzi ya WorldSkills Tanzania 2026 yameanza leo, Agosti 20, 2026 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara jijini Tanga ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea mkoani humo.


Mashindano hayo yanawakutanisha jumla ya vijana 46 wenye ujuzi mbalimbali wakionesha uwezo wao katika fani tofauti za ufundi na ubunifu, huku yakilenga kutambua, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana pamoja na kuwaandaa kushindana katika viwango vya kimataifa. 


Tanzania inashiriki mashindano hayo ikiwa ni sehemu ya hatua za kuimarisha mafunzo ya ujuzi na kuwaunganisha vijana na fursa za ajira na kujiajiri, ambapo mashindano hayo yanatarajiwa pia kuwa jukwaa la kuonesha namna ujuzi na ubunifu wa vijana unavyoweza kubadilishwa kuwa bidhaa na huduma zenye thamani, kuongeza uzalishaji wa ndani na kuchangia uchumi wa taifa.


‎Mashindano hayo yanaratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.







No comments:

Post a Comment