MHE. MAHUNDI ASHIRIKI MAPOKEZI YA MWAKILISHI WA MWENYEKITI WA UWT TAIFA KATIKA ZIARA YA KIKAZI CHUNYA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, August 5, 2026

MHE. MAHUNDI ASHIRIKI MAPOKEZI YA MWAKILISHI WA MWENYEKITI WA UWT TAIFA KATIKA ZIARA YA KIKAZI CHUNYA


Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, ameshiriki mapokezi ya Mhe. Dkt. Catherine Canute aliyemwakilisha Mwenyekiti wa UWT Taifa katika ziara ya kikazi Wilaya ya Chunya.

Ziara hiyo imelenga kukagua uhai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2025/2030 na namna miradi ya maendeleo inavyotekelezwa katika wilaya hiyo.

Akizungumza katika kikao cha kupokea na kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa kazi za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), pamoja na taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, Mhe. Dkt. Catherine Canute amewapongeza viongozi wa Chama, wakiwemo wabunge na viongozi wa Serikali, kwa ushirikiano wao katika kusimamia na kuharakisha maendeleo ya Wilaya ya Chunya.

Aidha, amempongeza Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo na juhudi zake katika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kuwanufaisha wananchi.

Pia amesisitiza wazazi na walezi kuhakikisha wanasimamia malezi bora kwa watoto na vijana ili kuwajenga katika maadili mema na kuwaandaa kuwa viongozi na wananchi wenye uwezo wa kuendeleza taifa imara la kesho.

Aidha, Mhe. Canute amempongeza Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo na jitihada zake katika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kuleta manufaa kwa wananchi.

Pamoja na hayo, amesisitiza wazazi na walezi kuendelea kusimamia malezi bora kwa watoto na vijana ili kuwajenga katika misingi sahihi itakayowawezesha kuwa chachu ya maendeleo na kuendeleza taifa lenye nguvu na imara.

Amesema ushirikiano wa viongozi pamoja na malezi bora kwa vijana ni nguzo muhimu katika kujenga jamii yenye uwajibikaji na maendeleo endelevu.

Kwa upande wake, Mhe. Mahundi ameendelea kusisitiza umuhimu wa mshikamano kati ya viongozi, Chama na wananchi katika kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaleta matokeo chanya kwa wananchi wa Chunya na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment