Na Mwandishi Wetu - Dodoma
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Sospeter Mtwale amewataka Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuendelea kutoa tabasamu kwa wananchi kwa kuwafikishia huduma bora za ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara.
Bw. Mtwale amesema hayo alipotembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya Kitaifa na Kimataifa ya Kilimo Nanenane 2026 yanayoendelea katika viwanja vya Dkt. John Samwel Malecela jijini Dodoma.
Amesema jitihada hizo zinaendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara ili iweze kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo kurahisisha usafirishaji wa mazao ya wakulima, bidhaa na huduma hivyo kuongeza fursa na kuboresha maisha ya wananchi.

No comments:
Post a Comment