NAIBU MTENDAJI SUMA JKT ATEMBELEA BANDA LA MALIASILI NANE NANE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, August 3, 2026

NAIBU MTENDAJI SUMA JKT ATEMBELEA BANDA LA MALIASILI NANE NANE


Na Neema Chalila Mbuja, Dodoma


NAIBU Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT Brigedia Jenerali Shija Lupi leo Agosti 03, 2026 ametembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kujionea wadau mbalimbali wanaoshirikiana na wizara kwenye uzalishaji wa bidhaa za misitu na asali na kuipongeza wizara kwa kushirikiana na wadau hao.

Brigedia Jenerali Shija amesema wadau hao wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika kuhakikisha mazao hayo ya bidhaa za nyuki ikiwemo asali, miche ya miti na mazao ya misitu yanakuwa na soko ndani na nje ya nchi.

Brigedia Jenerali Shija alipata wasaa wa kutembelea wanyamapori hai waliopo kwenye Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kama njia mojawapo ya kuutangaza utalii wa ndani.

No comments:

Post a Comment