Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dennis Simba, akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 20,2026 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa mamlaka hiyo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2025/26 na mwelekeo wa 2026/27.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
JUMLA ya zabuni 397,395 zenye thamani ya Sh40.4 trilioni zimetolewa kupitia Mfumo wa Ununuzi wa Umma Kielektroniki (NeST), huku makundi maalum yakinufaika na zabuni zenye thamani ya Sh56 bilioni tangu mfumo huo ulipoanza kutumika.
Hayo yamesemwa leo Agosti 20,2026 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dennis Simba,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mamlaka hiyo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2025/26 na mwelekeo wa 2026/27.
Simba amesema matumizi ya NeST yameleta mabadiliko makubwa katika sekta ya ununuzi wa umma kwa kuongeza uwazi, ushindani, ufanisi na uwajibikaji, huku pia yakirahisisha upatikanaji wa fursa za zabuni kwa wazabuni kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Amesema takribani asilimia 70 ya bajeti ya Serikali hutumika kupitia ununuzi wa umma, jambo linaloifanya sekta hiyo kuwa eneo muhimu la fursa za biashara na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Ukidhi wa sheria wapanda Kwa mujibu wa Simba, matumizi ya NeST yameongeza kiwango cha uzingatiaji wa sheria katika michakato ya ununuzi wa umma kutoka asilimia 65 mwaka 2023/24 hadi asilimia 76 mwaka 2024/25 na kufikia asilimia 79 mwaka 2025/26.
Amesema mfumo huo pia umepunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya karatasi, ambapo zaidi ya kurasa milioni 288.57 za nyaraka za zabuni zimeepukwa kuchapishwa, hatua iliyookoa takribani Sh27.64 bilioni.
“Hivi sasa, mzabuni anaomba zabuni popote alipo,” amesema Simba, akieleza kuwa mfumo huo umeondoa ulazima wa wazabuni kusafiri kupeleka nyaraka za zabuni katika taasisi nunuzi.
Amesema hatua hiyo imepunguza gharama na muda wa wazabuni kushiriki katika michakato ya ununuzi wa umma.
NeST yaunganishwa na mifumo zaidi ya 30 Simba amesema NeST, ambao ulianza kutumika rasmi mwaka 2023, umeunganishwa na mifumo zaidi ya 30, ikiwemo mifumo ya benki, malipo, mifuko ya hifadhi za jamii, bodi za usajili wa wataalamu na mifumo ya leseni.
Amesema hatua hiyo imeongeza ufanisi wa uhakiki wa taarifa na nyaraka, huku ikisaidia kuondoa uwezekano wa matumizi ya nyaraka za kughushi kwenye michakato ya zabuni.
Kwa upande wa usimamizi wa mikataba, amesema mchakato wa uhakiki na usainishaji wa mikataba sasa unaweza kufanyika kidigitali ndani ya NeST bila kuchapisha nyaraka.
Aidha, amesema PPRA imeanza kuunganisha mfumo huo na benki kwa ajili ya kuhakiki dhamana za zabuni, ambapo NMB tayari imeshirikiana na PPRA huku TCB na CRDB zikiwa katika hatua za mwisho za kuunganishwa.
Amesema Bank Security Portal nayo ipo katika hatua za mwisho za majaribio na inatarajiwa kuanza kutumika kufikia mwisho wa robo ya mwaka wa fedha, hatua itakayopanua huduma hiyo kwa benki zote.
Makundi maalum yapewa fursa Simba amesema Sheria ya Ununuzi wa Umma inaelekeza taasisi za umma kutenga asilimia 30 ya bajeti zao za ununuzi kwa ajili ya makundi maalum, yakiwemo vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu.
Amesema hadi sasa makundi maalum 27,946 yamesajiliwa kwenye NeST.
Kati ya hayo, vijana ni 13,317, wanawake 13,400, wazee 643 na watu wenye ulemavu 586.
Makundi hayo, amesema, yamekwishapata zabuni zenye jumla ya thamani ya Sh56 bilioni kupitia mfumo huo.
PPRA inalenga kuongeza idadi hiyo hadi kufikia takribani makundi 300,000 yaliyo tayari kushiriki katika zabuni za umma, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Simba amesema hatua hiyo inalenga pia kutoa fursa za ajira na kipato kwa Watanzania ambao huenda wasiwe na uwezo wa kuanzisha kampuni, lakini wanaweza kuungana katika vikundi na kushiriki katika zabuni.
Kwa mujibu wa PPRA, kundi maalum linaweza kupata zabuni moja yenye thamani ya hadi Sh500 milioni.
“Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa tunakuwa na uchumi jumuishi; kwamba kila Mtanzania ananufaika na anachangia pia kwenye ukuaji wa uchumi katika ngazi yoyote aliyopo,” amesema.
Amesema PPRA, kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – Wizara ya Maendeleo ya Vijana, itazunguka katika Halmashauri zote 184 nchini kutoa elimu na kuhamasisha usajili wa vikundi.
Zabuni za hadi Sh50 bilioni kwa wazawa Simba amesema Sheria ya Ununuzi wa Umma imeweka upendeleo kwa wazabuni na bidhaa za ndani, ambapo zabuni zote zenye thamani isiyozidi Sh50 bilioni zimetengwa kwa wazawa pekee.
Aidha, amesema wazabuni wa ndani wanaweza kupata upendeleo wa hadi asilimia 10 katika zabuni zinazohusisha ushindani wa kimataifa, huku bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi zikipata upendeleo wa hadi asilimia 15 dhidi ya bidhaa kutoka nje.
Amesema mfumo wa NeST umewezesha utekelezaji wa upendeleo huo kwa njia ya kidigitali, ikiwemo kuzuia wazabuni wa nje kuomba zabuni zilizotengwa kwa wazawa.
Programu ya NeST Tenderer Katika hatua nyingine, PPRA imeanzisha programu ya simu inayojulikana kama NeST Tenderer, inayopatikana kupitia Play Store na App Store.
Simba amesema programu hiyo inalenga kuwafikishia wananchi fursa za zabuni za umma moja kwa moja kupitia simu janja.
Mtumiaji anaweza kujisajili kwenye NeST, kuomba zabuni na kufuatilia malipo yake kupitia programu hiyo.
Mfumo watambuliwa kimataifa Simba amesema ubora wa NeST umetambuliwa ndani na nje ya Tanzania, ambapo Novemba 2024 mfumo huo ulishinda tuzo ya “Mfumo Bora Zaidi wa Ununuzi wa Umma Barani Afrika” katika tuzo za African Association for Public Administration and Management (AAPAM) zilizofanyika Kampala, Uganda.
Amesema mwaka huu, 2026, NeST pia umetambuliwa miongoni mwa mifumo 20 bora ya Serikali Mtandao duniani katika tuzo za World Summit on the Information Society (WSIS) Prizes 2026, zilizofanyika Julai 8, 2026, Geneva, Uswisi.
Amesema kutokana na mafanikio hayo, Tanzania imekuwa ikipokea wageni kutoka nchi mbalimbali za Afrika, zikiwemo Uganda, Rwanda, Burundi, Botswana na Sudan, kwa ajili ya kujifunza uzoefu wa Tanzania katika usimamizi wa ununuzi wa umma.
PPRA yajenga uwezo wa zaidi ya watu 160,000 Simba amesema katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili 2026, Serikali kupitia PPRA imewajengea uwezo wadau mbalimbali wa ununuzi wa umma.
Amesema watumishi 124,657 kutoka taasisi nunuzi wamepatiwa mafunzo, pamoja na wazabuni zaidi ya 12,973 na washiriki zaidi ya 11,891 kutoka makundi maalum.
Aidha, wanafunzi 560 wa vyuo vya elimu ya juu, washiriki 9,637 kutoka taasisi za ngazi za chini za Serikali, zaidi ya 100 kutoka asasi za kiraia, wabunge 393 pamoja na wahariri na waandishi wa habari 929 wamepatiwa elimu kuhusu ununuzi wa umma.
Simba amesema PPRA pia imeendelea kutumia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, vipindi vya redio na televisheni pamoja na sanaa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu fursa za ununuzi wa umma.
Amesema mwaka jana PPRA iliandaa vipindi maalum 17 vya redio vilivyorushwa na zaidi ya vituo 12, huku pia ikiandaa filamu ya elimu iitwayo “Winga.”

No comments:
Post a Comment