SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA UANDAAJI WA MIPANGO NA BAJETI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, August 20, 2026

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA UANDAAJI WA MIPANGO NA BAJETI

Mhasibu Mkuu Msaidizi wa Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Ayubu Banzi, akifungua kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa wataalamu wa Mipango na Bajeti kundi la pili kati ya makundi matatu yanayoshiriki mafunzo ya Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa watalaam kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali na sekretarieti za mikoa na mamlaka ya Serikali za mitaa, kinachofanyika Treasury Square Dodoma.
Meza Kuu ikiongozwa na Mhasibu Mkuu Msaidizi wa Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Ayubu Banzi, katika kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa wataalamu wa Mipango na Bajeti kundi la pili kuhusu Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa watalaam kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali na sekretarieti za mikoa na mamlaka ya Serikali za mitaa, kinachofanyika Treasury Square Dodoma, kushoto ni Kaimu Kamishna wa Idara ya Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Raymond Kwohelera na kulia ni Kamishna Msaidizi Idara ya Bajeti Bw. Fundi Makama.
Kamishna Msaidizi Idara ya Bajeti Bw. Fundi Makama, akiwakaribisha watalaam kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali na sekretarieti za mikoa na mamlaka ya Serikali za mitaa, katika kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa, kinachofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma.
Afisa Msamimizi wa Fedha Mwandamizi Idara ya Usimamizi wa Bajeti Wizara ya Fedha, Bi. Tunsume Mlawa, akieleza kuhusu tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa watalaam kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali na sekretarieti za mikoa na mamlaka ya Serikali za mitaa, kinachofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma.
Meza kuu ikiongozwa na Mhasibu Mkuu Msaidizi wa Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Ayubu Banzi, Kaimu Kamshina wa Idara ya Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Raymond Kwohelera na Kamishna Msaidizi wa Idara hiyo, Bw. Fundi Makama, wakiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa Kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti, kinachofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma.
Baadhi ya Washiriki wa kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa watalaam kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali na sekretarieti za mikoa na mamlaka ya Serikali za mitaa, wakifuatilia mada, 1katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)


Na. Farida Ramadhani na Saidina Msangi, WF, Dodoma


Serikali imeeleza kuwa inaendelea kuboresha uandaaji wa mipango na bajeti ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji na usimamizi wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2027/28–2029/30.

Hayo yameelezwa katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma na Mhasibu Mkuu Msaidizi wa Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Ayubu Banzi, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, wakati akifungua kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa wataalamu wa Mipango na Bajeti kundi la pili kati ya makundi matatu yanayoshiriki mafunzo hayo.

Bw. Banzi alisema kikao hicho ni muhimu kwa kuwa kitatoa fursa kwa washiriki kutoa maoni yatakayotumika kuboresha na kuongeza ufanisi katika utekelezaji na usimamizi wa bajeti ya Serikali.

Alisema maoni hayo pia yatasaidia kuboresha Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2027/28–2029/30.

Kikao hicho kimewahusisha wataalamu wa masuala ya mipango na bajeti kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Lengo la kikao hicho ni kuhakikisha kuwa wataalamu wanaendelea kuwa na uelewa na uwezo unaohitajika katika maandalizi, utekelezaji na usimamizi wa mipango na bajeti ya Serikali.

No comments:

Post a Comment