Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), amesisitiza umuhimu wa kuimarisha Ushirikiano kati Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) katika kuongeza uwekezaji na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maji nchini.
Ameyasema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya Wizara ya Maji katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kuhusu mgawanyo wa fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia mwaka 2024 hadi 2025.
Waziri Aweso amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi, sambamba na kushirikisha sekta binafsi na wadau mbalimbali katika kuongeza uwekezaji na kuboresha huduma za maji nchini.
Amesisitiza umuhimu wa kukamilisha miradi ya maji vijijini, kwasababu Serikali inalenga kumaliza uhaba wa maji katika vijiji 1,575 ambavyo bado havijafikiwa na miundombinu ya huduma ya maji.
Waziri Aweso amesisitiza matumizi bora ya fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji kwa kuzielekeza katika maeneo yenye mahitaji makubwa, na kutaka utekelezaji wa miradi uzingatie thamani ya fedha kwa kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa kwa manufaa ya wananchi.








No comments:
Post a Comment