Na Mwandishi Wetu - Dodoma
Nchi wanachama wa Bonde la Mto Nile zinakabiliwa na changamoto zinazoongezeka za upatikanaji na usimamizi wa rasilimali za maji kutokana na mabadiliko ya tabianchi, ongezeko la watu, ukuaji wa uchumi na kuongezeka kwa mahitaji ya maji, chakula na nishati, huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa Jukwaa la Nane la Wadau wa Maendeleo ya Bonde la Mto Nile (NBDF8) kwa ajili ya kutafuta suluhisho la pamoja.

Jukwaa hilo limezinduliwa rasmi jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, kwa niaba ya Waziri wa Maji, likiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano miongoni mwa nchi washirika wa Bonde la Mto Nile katika kutafuta suluhisho bunifu za kugharamia miundombinu ya maji pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhandisi Mwajuma amesema Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa jukwaa hilo kutokana na nafasi yake muhimu katika Bonde la Mto Nile, akieleza kuwa Ziwa Victoria, ambalo ni chanzo kikubwa cha Mto Nile, kwa sehemu kubwa linapatikana nchini Tanzania.
Amesema changamoto zinazolikabili Bonde la Mto Nile zinaendelea kuongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi, ongezeko la idadi ya watu na matumizi ya rasilimali, ukuaji wa uchumi pamoja na mahitaji yanayoongezeka ya maji, chakula na nishati.
Kwa mujibu wa Mhandisi Mwajuma, hali hiyo inaongeza umuhimu wa nchi wanachama kuimarisha ushirikiano katika kulinda, kuendeleza na kusimamia kwa pamoja rasilimali za maji zinazoshirikishwa na nchi hizo.
Amesema ushiriki wa Tanzania katika shughuli za Bonde la Mto Nile tayari umeleta mafanikio mbalimbali, ikiwemo kuboreshwa kwa vituo vinane vya kitaifa vya ufuatiliaji wa taarifa za maji katika Bonde la Ziwa Victoria.
Mafanikio mengine, amesema, ni matumizi ya teknolojia za kisasa za mawasiliano katika ukusanyaji wa taarifa za maji, upatikanaji wa vifaa vya kufuatilia ubora wa maji na maji ya chini ya ardhi, pamoja na taarifa zinazohusiana na nishati ya umeme.
Ameeleza kuwa Jukwaa la Nane la Wadau wa Maendeleo ya Bonde la Mto Nile litatekelezwa kupitia shughuli mbalimbali, zikiwemo uwasilishaji wa tafiti, semina za mtandaoni na kampeni za uhamasishaji wa umma.
Aidha, amesema kutakuwa na mkutano mkuu utakaofanyika jijini Dar es Salaam, utakaowakutanisha wataalamu na viongozi mbalimbali kwa ajili ya mijadala ya kitaalamu na kubadilishana uzoefu kuhusu maendeleo na usimamizi wa rasilimali za Bonde la Mto Nile.
Mhandisi Mwajuma amewaalika wataalamu wa maandiko pamoja na waandishi wa habari kushiriki kikamilifu katika jukwaa hilo kwa kuwasilisha tafiti, makala na habari zinazohusu Bonde la Mto Nile, ambazo zitashindanishwa na washindi kutunukiwa tuzo.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Bonde la Nile, Mhandisi Nestor Niyonzima, amewataka wadau mbalimbali kutumia fursa hiyo kuwasilisha maandiko na habari zinazohusu Bonde la Mto Nile kwa lugha mbalimbali, ikiwemo Kiswahili.
Amesema ushiriki mpana wa wataalamu, waandishi wa habari na wadau wengine ni muhimu katika kuongeza uelewa wa umma kuhusu umuhimu wa rasilimali za maji na kuibua mijadala itakayosaidia nchi za Bonde la Mto Nile kupata suluhisho la changamoto zinazolikabili.
Jukwaa hilo linatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya kuimarisha ushirikiano wa nchi washirika wa Bonde la Mto Nile katika kuhakikisha rasilimali za maji zinatumika kwa njia endelevu, huku zikizingatia mahitaji ya sasa na ya vizazi vijavyo.

No comments:
Post a Comment