Na Saidi Saidi, WMJJWM – Dodoma
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, amemkabidhi bajaji mpya Pius Patrick, mkazi wa Ipagala jijini Dodoma, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni utekelezaji wa ombi la msaada alilowasilisha kupitia Ofisi ya Rais.
Dkt. Gwajima amekabidhi bajaji hiyo Agosti 4, 2026, akieleza kuwa Serikali itaendelea kuwagusa wananchi wenye mahitaji mbalimbali kwa kuwapatia msaada unaowawezesha kujitegemea na kuboresha maisha yao.
Pius aliomba msaada huo baada ya kupata changamoto za kiafya zilizotokana na ajali iliyosababisha kuvunjika miguu. Bajaji hiyo itamwezesha kurahisisha usafiri wake wa kila siku na kujiongezea kipato kupitia shughuli za kiuchumi.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Dkt. Gwajima alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali na kutimiza ombi la Pius, akisema hatua hiyo inaonesha dhamira ya Serikali ya kuendelea kuwahudumia wananchi na kuwapa matumaini, hususan wenye mahitaji maalum.
Kwa upande wake, Pius Patrick alimshukuru Rais Samia pamoja na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kutimiza ombi lake. Amesema ataitunza bajaji hiyo na kuitumia ipasavyo kama nyenzo ya kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yake.









No comments:
Post a Comment