BARRICK BULYANHULU YAKABIDHI JENERETA KUBWA LA KISASA KITUO CHA AFYA BUGARAMA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, September 20, 2026

BARRICK BULYANHULU YAKABIDHI JENERETA KUBWA LA KISASA KITUO CHA AFYA BUGARAMA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI

Afisa Mahusiano ya Jamii kutoka Barrick Bulyanhulu, Stella Kuyonga (katikati) akingalia zoezi la ufungaji jenereta katika kituo cha afya cha Bugarama ambalo limekabidhiwa na mgodi kusaidia kukabiliana na changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara na kuathiri utoaji huduma kwa wananchi.
Afisa Mahusiano ya Jamii kutoka Barrick Bulyanhulu, Stella Kuyonga akingalia zoezi la ufungaji jenereta katika kituo cha afya cha Bugarama ambalo limekabidhiwa na mgodi kusaidia kukabiliana na changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara na kuathiri utoaji huduma kwa wananchi.
Muonekano wa jenereta lililokabidhwa na Barrick Bulyanhulu katika kituo cha afya cha Bugarama

Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Bugarama kilichopo kata ya Bugarama  halmashauri ya Msalala  Dkt. Silasi Kayanda akizungumza.
Mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo Halmashauri ya wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga unaendelea kuunga mkono jitihada za serikali kuboresha sekta ya afya kupitia ufanikishaj miradi ya kutatua kero mbalimbali kwa wananchi wa maeneo yanayouzunguka mgodi huo.

Kupitia fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) umekabidhi jenereta kubwa ya kisasa katika kituo cha afya Bugarama kilichopo kata ya Bugarama  halmashauri ya Msalala kwa ajili ya kutatua changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara, jambo lililokuwa likikwamisha huduma muhimu kama upasuaji na huduma za chumba cha kuhifadhi maiti (Mortuary).

Akiongea wakati wa kukabidhi jenereta hiyo kwa niaba ya Mgodi, Afisa Mahusiano ya Jamii kutoka Barrick Bulyanhulu, Stella Kuyonga alisema jenereta hiyo ina uwezo wa KVA 66 na ina thamani ya shilingi milioni 66.7

“Jenereta hii imetolewa ikiwa ni mwendelezo wa kusaidia changamoto mbalimbali zinazokwamisha huduma bora katika kituo hicho ambacho kinahudumia idadi ya wananchi kutoka maeneo yanayozunguka mgodi na sehemu nyinginezo za mbali ikiwemo Geita. Barrick inathamini suala la usalama na afya katika jamii ndio maana imelipa kipaumbele kikubwa suala hili la utatuzi wa changamoto ya kusimama huduma kutokana na kukatika umeme”, alisema Kuyonga.

Kwa Upande wake Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dkt. Silasi Kayanda ameishukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kukipatia kituo jenereta hiyo ambayo itawezesha uhakika wa huduma za upasuaji wa wagonjwa, kuwapa joto watoto njiti pamoja na huduma ya kuhifadhi maiti.”Jenereta hii imepatikana katika wakati mwafaka itasaidia kuimarisha huduma na kuokoa maisha ya wagonjwa” alisema Kayanda.

Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umefanya uwekezaji mkubwa katika kituo cha afya Bugarama kwa kujenga miundombinu hali ambayo imekiwezesha kutoa huduma bora mbalimbali za afya kwa wananchi ikiwemo wodi ya kujifungua kwa wakinawawa ambapo kwa sasa kinahudumia zaidi ya wananchi 50,000 kwa mwaka.

Mbali na kukabidhi jenereta la kisasa Barrick pia mwaka juzi ilikipatia kituo hicho gari la wagonjwa (ambulance) ambalo linaendelea kusaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji rufaa ya haraka vilevile ilitoa mashine ya kisasa za maabara (Biohazard Safety Cabinet kwa ajili ya kuboresha usalama na ufanisi wa vipimo vya kimaabara kituoni hapo.

Baadhi ya wananchi wanaonufaika na huduma za kituo cha afya Bugarama walieleza kuwa wanaendelea kufurahia uboreshwaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika maeneo yao kutokana na fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) zinazotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.

Neema Rafaeli mkazi wa Kakola mwenye watoto watano alisema uwepo wa mgodi katika eneo lao umesaidia kuimarisha huduma mbalimbali kwa wananchi hasa afya ambapo huduma za akina mama za kujifungua hivi sasa zimekuwa nzuri kutokana na mgodi wa Barrick kushirikiana na Serikali kufanikisha ujenzi wa kituo cha afya Bugarama kinachowezesha wananchi kupata huduma bora za afya.

Mgodi wa Barrick Bulyanhulu pia umekuwa mstari wa mbele kufanikisha miradi ya elimu,uchumi,uwezeshaji wa wananchi, maji na miundombinu ya barabara ambapo kwa sasa kwa kushirikiana na mgodi wa Barrick North Mara unatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara ya Kahama mpaka Kakola kwa kiwango cha lami ambayo ujenzi wake ukikamilika utarahisisha usafiri kwa wananchi na mizigo, kurahisisha shughuli za kiuchumi, na kufungua fursa za maendeleo katika mkoa wa Shinyanga na maeneo jirani.

No comments:

Post a Comment