NOMBO: VIONGOZI WA ELIMU SIMAMIENI MITIHANI KWA UMAKINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 8, 2026

NOMBO: VIONGOZI WA ELIMU SIMAMIENI MITIHANI KWA UMAKINI



Serikali imesema udanganyifu katika mitihani ya kitaifa umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kuimarishwa kwa usimamizi wa mitihani nchini.

Kauli hiyo imetolewa Septemba 7, 2026 mkoani Ruvuma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Prof. Carolyne Nombo, alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na kuazungumzia utekelezaji wa masuala mbalimbali ya elimu ikiwemo maandalizi ya mtihani wa Taifa wa darasa la saba unaotrajia kufanyika nchini kote Septemba 9 na 10, 2026.

Ameeleza kuwa mitihani ya kitaifa ni suala nyeti linalohitaji usimamizi madhubuti, hivyo viongozi wa elimu katika ngazi zote wanapaswa kuhakikisha taratibu zote za mitihani zinafuatwa.

“Udanganyifu umepungua kwa kiasi kikubwa, nawasihi wanafunzi wa darasa la saba manaotarajia kufanya mitihani yenu kutojiingiza katika udanganyifu wowote wa mitihani, tuzingatie taratibu zote za mitihani,” amesisitiza Prof. Nombo

Aidha, amezitaka kamati za mitihani za mikoa na viongozi wa elimu kuendelea kushirikiana katika kusimamia mitihani, huku akiwapongeza kwa hatua ambazo tayari zimechukuliwa katika kupunguza udanganyifu.

Amebainisha kuwa, Serikali itaendelea kuchukua hatua pale inapobaini vitendo vya udanganyifu, hasa vile vinavyohusisha kupanga kwa pamoja kati ya wanafunzi, walimu au wasimamizi wa mitihani.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Songea Mhe. Wilman Kapenjama amesema mkoa umejiandaa vema katika kusimamia mtihani huo kwa hali ya usalama bila changamoto yoyote.

No comments:

Post a Comment