Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndg. Rabia Abdalla Hamid (MCC), amesisitiza umuhimu wa kila mwananchi kutimiza wajibu wake katika kudumisha umoja, mshikamano, amani na utulivu nchini.
Ndg. Rabia ameyasema hayo leo Septemba 22, 2026, baada ya kupokelewa katika Ofisi za CCM Mkoa wa Morogoro, ambapo ametembelea vikundi vya wajasiriamali na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi, huku baadhi ya changamoto hizo zikitatuliwa papo hapo.
Aidha, Ndugu Rabia ametumia nafasi hiyo kuzungumza na makundi mbalimbali ya kijamii, akisisitiza kuwa amani, umoja na mshikamano ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa na ustawi wa wananchi.
Amesema kila mwananchi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana wajibu wa kulinda na kudumisha amani, utulivu, umoja na mshikamano kwa maslahi ya Watanzania wote.
Amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kushirikiana na Serikali pamoja na taasisi mbalimbali katika kutatua changamoto zinazowakabili na kujenga jamii yenye mshikamano na mazingira rafiki kwa maendeleo.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)




No comments:
Post a Comment